SERIKALI IMEAGIZA MABEHEWA ILI KUKAMILISHA MRADI WA RELI YA KISASA

Serikali imeagiza Mabehewa elfu moja mia nne na themanini ikiwa ni hatua ya kukamilisha mradi wa Reli ya kisasa unaoendelea.
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo na msemaji mkuu wa Serikali dkt Hassan Abas wakati akizungumzia hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika kipindi cha miaka ya miaka minne tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.
Amesema Serikali imetekeleza miradi katika sekta za elimu kwa kutoa elimu bure na kutoa kias kikubwa cha fedha ili kuiwezesha sekta hiyo kujiendesha pamoja na ujenzi wa majengo ya madarasa, mabweni zaidi ya 500 na kukarabati shule kongwe 65 kwa zaidi ya shilingi bilioni 70 pamoja na kuongeza ajira kwa wataalamu wa afya.
Aidha Serikali imeendelea na jitihada zake za ununuzi wa Ndege, utekelezaji wa miradi mikubwa 300 kwenye sekta za miundo mbinu ya barabara, umeme, na maji kwa fedha za ndani na hivyo kutokukamilika kwa baadhi ya miradi imetokana na taratibu za kiuhandisi na si kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Dkt Abas akafafanuaa kuwa hatua hiyo imechangiwa na mwamko wa watanzania juu ya ulipaji wa kodi, ambapo pia kuhusu rushwa amesema tanzania sasa ni miongoni mwa nchi zinazojulikana duniani kwa kupiga vita rushwa kwa vitendo.

Comments are closed.

error: Content is protected !!