Blog

VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM WAMETAKIWA KUACHA SIASA ZA KUGOMBANA KATIKA KUGOMBEA UONGOZI

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt.John Pombe Magufuli amewataka Viongozi na Wanachama wa Chama hicho kuacha siasa za kugombana katika kugombea Uongozi hasa katika nafasi za Ubunge na Udiwani.

Amesema kutokana na uimara wa Chama hicho ni maslahi yake yawekwe mbele ya Chama hicho na wakati ukifika wanaonyesha nia watatangazwa na kufuata taratibu kwa kila hatua.

Dkt.Magufuli amesema ni muhimu kuhakikisha wanakuwa na uomja na mshikamano na  kutowakatisha tamaa Wanachama waliotayari kutumikia Chama hicho au kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM.

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Nd. John Kijazi amesema uteuzi huo Dkt. Magufuli amemteuwa Mhe. Mussa Hassan Zungu kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira na Mhe. George Simbachawene anachukuwa nafasi ya  Kangi Lugola aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae nafasi yake imetenguliwa kuanzia leo.

Pia Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna Jenereli wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias andengenye ambaye nafasi yake itajazwa baadae.

Pia Dk Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi watatu ambao wanawakilisha Tanzania katika Nchi mbali mbali ambapo Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na Mabalozi waliokuwa katika vituo hivyo kumaliza muda wao.

Vituo vya Mabalozi hao watatu walioteuliwa vitatangazwa baadae.

Pia Dk. Magufuli ameitaka Takukuru kufanya uchunguzi  kuhusiana na Mkataba uliosainiwa na Kampuni kutoka Nje ya Nchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaogharimu zaidi ta Shilingi Trilioni Moja ambao unadaiwa hauna tija kwa Nchi.

UBOVU WA BARABARA ILIYOKUWA IKIWAKABILI WANANCHI WA VULENI WILAYA YA CHAKE CHAKE LIMEPATIWA UFUMBUZI

 

Tatizo la Usafiri la muda mrefu ambao unachangiwa na ubovu wa Barabara uliyokuwa ukiwakabili Wananchi wa Vuleni Wilaya ya Chake Chake limepatiwa uvumbuzi kwa kuanza ujenzi wa Barabara hiyo.

Wakizungumza katika Ujenzi wa Barabara hiyo baadhi ya Wananchi wamesema kujengwa kwa Barabara hiyo na Baraza la Mji Chake kutawasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na tatizo  hila kwani wmekuwa wakishindwa hata kusafirisha bidha zao.

Mapema Mhandisi wa Barabara hiyo Nd. Mohammed Mzee Mohammed amesema ujenzi wa Barabara hiyo utajengwa kwa kiwango cha kifusi ukiwa na urefu wa 250 na ukitarajiwa kumalizika ndani ya wiki moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Mji Chake Chake Nd. Salma Abuu Hamad amesema ujenzi wa Barabara hiyo nikatika kuondoshea changamoto za Barabara zinazo wakabili Wananchi na kuwaletea maendeleo .

BARAZA LA MANISPAA MAGHARIB A LIMESEMA LITAENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Magharib "A"  Nd. Rashid Mohammed Mahmood amesema atashirkiana na watendaji wa Baraza hilo ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Wilaya hiyo.

Akizungumza baada ya kuapisha kuwa Meya wa Halmashauri hiyo Mstahiki Meya huyo amesema nguvu za pamoja katika kutekeleza majukumu ya kila siku yatawezesha kufanikisha mipango wanayojiwekea.

Msahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Nd.  Saleh Juma Kinana  amesema yupo tayari kushirikiana pamoja na uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuimarisha huduma za usafi katika Miji yote Nchini.

 

error: Content is protected !!