Blog

BARAZA LA USIMAMIZI NA UTOAJI WA LESENI KUANDAA MFUMO BORA WA UTOAJI WA LESENI

Waziri  wa biashara  na  viwanda  Balozi Amina Salum  Ali  ameliagiza Baraza  la  usimamizi  na  utoaji wa  leseni  kuandaa mfumo bora  wa utoaji wa leseni  ili  kuwapunguzia  wafanyabiasha mzigo  wa   utitiri  wa  tozo  mbali  mbali.

Balozi amina  ametoa  agizo  hilo  wakati  akizindua  bodi  ya  taasisi  hiyo  yenye dhamana  ya  kusimamia  leseni , amesema  kumekuwa  na tozo  nyingi  zinazotolewa  na  taasisi mbali mbali jambo linalowaongezea  gharama  wafanyabiashara  na  wanachi  kwa  kupanda  kwa  bei.

Amewasisitiza  wajumbe  wa  bodi  hiyo  kukaa  pamoja  na  kuandaa mfumo  utakaofanya  leseni  kutolewa  katika  kituo  kimoja na  kuachana  na  utaratibu  uliopo  sasa  kwa baadhi ya taasisi kufanya majukumu yanayofanana katika sekta moja.

Mwenyekiti  wa  bodi  hiyo  nd,  Vuai  Mussa  ameahidi  kwa  wajumbe  wa  bodi  hiyo  kutekeleza  majukumu  waliokabidhiwa  kwa  umakini  na  uadilifu  pamoja na matatizo yaliyopo na  dhamira  na  malengo  ya  Serjkali  katika  kuimarisha  sekta   ya  biashara.

 

MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA NCHI 16 WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Katibu mkuu wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto nd Zainabu Abdi Chaula amefungua mkutano wa makatibu wakuu wa nchi 16 wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC)ambao utajadili   agenda 13 ikiwemo kifua kikuu na ukimwi .

Akifungua mkuatano huo Bi Zainabu Chaula amesema mkutano huo umewashirikisha  makatibu wakuu kutoka nchi 16 za   SADC ambapo  utajadili masuala mbalimbali ya afya ambapo amebainisha kuwa malengo ya SADC kuwa ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa kifua kikuu uwe umeisha katika nchi za kusini mwa afrika .

Amezitaja agenda ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo ambao  utaongozwa na sekretariet ya sadc ni pamoja na masuala ya ukimwi, maambukizi ya virusi vya ukimwi ,tb,chanjo,malaria masuala ya lishe kuimarisha mifumo ya afya, huduma za afya ya uzazi pamoja na kupunguza vifo kwa mama wajawazito.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa tacaids dkt. Leonard Maboko amesema tanzania imefanya vizuri katika masuala ya tohara kwa wanaume ukilinganisha na nchi 16 za sadc.

Pia amesema mkutano huo  utajadili mambo ambayo yatasaidia kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kutoa elimu kwa makundi mbali mbali.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni ushirikiano wa nchi za sadc ni nguzo kuu ya kufikia maelendeo endelevu ya sekta ya afya na mapambano dhidi ya ukimwi

MAOFISA KUFANYA UCHUNGUZI KATIKA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA USHAHIDI WA VITENDO VYA UDHALILISHAJI.

Maofisa wa uchukuaji wa sampuli za vinasaba katika hosptali ya rufaa Mnazi Mmoja wamesisitizwa kufanya uchunguzi kwa umakini katika ukusanyaji wa taarifa za ushahidi wa vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumza na maofisa hao katika mafunzo yaliondeshwa na Afisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi  Dr  Salim Rashid amesema umakini utasaidia kuwa na taarifa za uhakika za kumtiia  hatiani mtuhumiwa katika kesi hizo zinazoripotiwa kila siku.

Amesema uwepo kwa mashine hiyo ya dna kutasaidia kurahisisha kazi za ushahidi katika vitendo vya udhalilishaji kwani na kuitaka jamiikuwa na uelewa pale tu zipanapotokezea kesi hizo.

Baadhi ya wafanyakazi wamesema mafunzo hayo yatawajengea ufanisi katika kazi zao na kuyataka yawe endelevu.

Mwanasheria wa maabara ya mkemia  Jabu Mabrouk na mtaalamu Gheda ali wamesema  katika uchukuaji wa sampuli kunahitajika kufuata taratibu maalum zinazohataji kuangaliwa makini ili kupata taarifa sahihi.

 

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUITANGAZA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi Bw. Hassan Khatib amevitaka Vyombo vya Habari kuisaidia Serikali katika kutangaza mambo mbalimbali ya maendeleo ili kuwavutia  wageni  na wenyeji.

Akizungumza na Wahariri na wamiliki wa Vyombo vya Habari amesema maendeleo  yapo masual mengi yaliyofanywa na kwa ajili ya wananchi hivyo  ni vyema kuyaelezea ili kuwatia moyo wananchi.

Mh. Hassan amekemea  tabia  ya baadhi ya watu wanovunja sheria kwa kutumia kivuli cha maendeleo na kuwataka kubadilika ili kuiweka nchi katika mazingira mazuri  kama zilivyo nchi nyengine duniani.

Nao Wahariri hao wa Vyombo vya Habari wamewaomba Viongozi wa Mkoa kuondosha urasimu kwa Waandishi wanaofuatilia matatizo yaliyomo katika maeneo yao yaliyokuwa kikwazo cha maendeleo kwa muda mrefu.

 

 

 

error: Content is protected !!