MWENYEKITI WA BODI YA ZBC AMEWATAKA WAFANYAKAZI KUIMARISHWA MAKTABA ZA SHIRIKA HILO

Mwenyekiti  wa   Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Bibi  Mahafoudha  Alley  Hamid  amesema  kuna  kila  sababu ya  kuimarishwa  kwa  Maktaba  za  Shirika  hilo  za  Redio  na  Television ili kuzuia  kupotea  kwa  hadhina kubwa  ya  vipindi , nyimbo  na  maigizo  vilivyohifadhiwa  katika maktaba  hizo.

Akizungumza na Uongozi na Wakuu wa Vitengo vya Shirika hilo  amesema Hali ya Mazingira za Maktaba za Shirika hilo  ni  chakavu  na  haziridhishi   hasa  kutokana na kuwa eneo hilo limekusanya kumbukumbu muhimu na  za miaka mingi iliopita .

Mwenyekiti Ummi amesisitiza kwa  Uongozi  na  Wafanyakazi  wa ZBC  kuzingatia  nidhamu  ya  Kazi , Ushirikiano na  Uzalendo  katika kutimiza  majukumu  waliopewa  na  Serikali  na  kamwe Bodi  hiyo  haitamvumilia  mtendaji  asiekuwa  tayari  katika   kutekeleza  majukumu  aliokabidhiwa .

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi wamewataka watendaji wa shirika hilo kuthamini juhudi za serikali hususan katika suala la kutunza rasilimali  za  shirika ambazo  zimegharimu  fedha  nyingi  ,

Wakitoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali baadhi ya Wakuu wa Vitengo  wameiomba  Bodi kuzipatia ufumbuzi  changamoto zinazo likabili shirika  ikiwemo  suala   sugu  la usafiri  na  fursa  za  Mafunzo.

Comments are closed.

error: Content is protected !!