MRADI WA ZOEZI LA UWEKAJI WA TAA ZA BARABARANI KWA UNGUJA NA PEMBA LINAENDELEA

 

Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Uwekaji wa Taa Barabarani Unguja na Pemba      Nd.Fadhil  Mlala amesema utekelezaji wake uko asilimia Arobaini tu kutokana na Watendaji wake kukwamishwa  na Mvua zinazoendelea  kunyesha .

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP  uliopangwa kukamilika  Mwezi  Mei Mwaka huu utagharimu Shilingi Bilioni Sita na Milioni Miatatu hadi  kukamilika kwake .

ZBC  imeshuhudia zoezi hilo likiwa likiendelea ambapo Bara bara  tano zenye kilomita kumi na nne zitawekwa  Taa Barabararani ikiwemo Kiembesamaki  Airpot  mpaka Mnazimmoja,   Mombasa  hadi  Kwerekwe.

Akielezea hatua inayotarajiwa kufanywa msimamizi wa mradi huo amesema ni kufunga taa mia mbili sitini na tano na amewataka Wananchi kulinda miundo mbinu baada ya kukamilika.

Nae  Msimmaizi Mkuu wa Taa hizo kutoka Manispaa Nd.Mcha Abdalla  Mussa  amesema Mradi huo  utatumia Umeme wa Jua na  Umeme kutoka Kidatu.

Kwa upande wake  Mkandarasi wa uwekaji wa Vitofali vya Taa Barabarani            Nd .Daudi  Lamek  Mabula amesema baadhi ya vifaa  viko  njiani vikotokea China kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo.

Comments are closed.

error: Content is protected !!