MRADI WA AFYA

Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mh Mattar Zahor Salim amesema tafiti zimeonesha kuwa vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 wamekabiliwa na matatizo ambayo yanaathiri ustawi wa maendeleo yao kiafya na kiakili.

Mh. Zahor amesema hayo huko katika ukumbi wa Baraza la mji Chake Chake wakati akizindua mradi wa wa Elimu ya Afya ya uzazi ,hiv,na lishe kwa vijana  utakaoendeshwa na Jumuiya ya ZAPHA+ na kufadhiliwa na UNICEF.

Mh. Zahor amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya kila  juhudi katika kuwanusu vijana kuingia katika tabia hatarishi na kupoteza muelekeo wa maisha yao ya baadae.

Kwa upande wao wawezeshaji katika uzinduzi huon nd. Hassan Mahmoud Ali ambae ni Afisa stadi za maisha na ushauri nasaha kutoka Wizara ya Elimu na  mratib wa tume ya ukimu Pemba nd. Nassor Ali Abdalla wamesema mradi huo  utawasaidia vijana katika kufahamu stadi za maisha kwani umri kati ya miaka 10 hadi 19 ndio kipindi hatari kwa vijana.

Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu mashirikiano ya pamoja  yahitajika  kati ya watendaji pamoja na wadau mbali ikiwemo Wizara ya Elimu pamoja na Masheha kwani Vijana  hao wamo  ndani ya  maeneo yao.

Comments are closed.