MRADI MPYA WA UJENZI WA BARABARA ZA WAPITA KWA MIGUU

Kampuni ya Ujenzi ya Advent Construction Limited imekabidhiwa Mradi mpya wa Ujenzi wa Barabara za wapita kwa miguu ili kuepusha Ajali kwa watembea kwa miguu na kupendezesha haiba ya Mji.

Akizungumza na ZBC Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mh. Rashid Simai Msaraka amesema  baraba hiyo ni kutoka  Mazizini hadi Maisara na wameitaka Kampuni hiyo kufanya Ujenzi huo kwa haraka  kulingana na maelekzo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini.

Engineer wa Kampuni ya Advent Construction  amesema Ujenzi huo utaanza hivi karibuni na wanatarajia kuchukua muda wa miezi minne hadi kumalizika kwake.

Mkuu wa  Mkoa wa Mjini ameipongeza Kampuni hiyo kwa mashirikiano makubwa   na kuonesha jitihada  za kuisaidia Serikali ya mapinduzi  katika kustawisha Jiji la Zanzibar.

Comments are closed.