MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATAKIWA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA KABLA YA KUTOA VIPIMO KWA WANANCHI

Waziri wa afya Mhe Hamad Rashida Mohamed ameitaka bodi ushauri  na wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa vipimo kwa wananchi ili kuepuka mifarakano katika jamii.

Hayo ameleza wakati akizidua bodi mpya  ambapo alitaka kutoa  elimu zaidi kwa wananchi pamoja na maskuli jinsi ya matumizi ya  kipimo cha DNA kwani wananchi walio wengi hawajuwi jinsi ya kipimo hicho kinavyo tumika.

Aidha alitaka  bodi hiyo kuvitunza vifaa hivyo muhimu ambavyo vimegharimu fedha nyingi ili viweze kudumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Mwenyekti  bodi hiyo Haji Mwamvura Haji amesema bodi hiyo itajikita zaid katika kufanya utafiti pamajia na kuwa wabunifu ili kuhakikisha kuwa lengo lilokusudiwa linanapatika  na kuhakikisha kuwa majibu yanayotolewa katika maabra yanakuna ni sahihi.

Nae mwenyekiti mstaafu wa bodi hiyo aliemaliza muda wake alishukuru mashirikiano aliyoyapata katika kufanya kazi zake na kuitaka bodi hiyo mpya kukaa pamoja na taasisi zinazohusiana na mambo ya sayansi ili kuweza kufanya kazi zao kwa uhakika zaidi.

No Comments Yet.

Leave a comment

error: Content is protected !!