MHE. MWANTATU AMESISITIZA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI KUFUATA SHERIA ZA KAZI ILI KUEPUKA MIGOGORO

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Mwantatu Mbarak Khamis Amesisitiza Waajiri na Wafanyakazi kufuata sheria za kazi ili kuepuka migogoro katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji ya Kamisheni ya Kazi, kwa kipindi cha Julai hadi Disember 2019 amesema Serikali imeweka Sheria hizo kwa taasisi za Serikali na Binafsi  ili kuweka taratibu na kanuni za utekelezaji wake.

Mapema Kamishna wa kazi Zanzibar Fatma Iddi Ali  akiwasilisha ripoti kwa kamati hiyo amesema Kamisheni imekagua taasisi 195 binafsi kufuatilia ulipaji wa kima kipya  cha mshahara ambapo taasisi 165 zinaendelea kulipa kima hicho, 30 zimepelekewa amri ya utekelezaji ambapo 23 zimetii amri, na saba zitapelekwa Mahakamani baada ya utaratibu wa sheria kukamilika.

Kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na ada ya vibali kwa wafanyakazi wa kigeni kwa mwezi wa Julai hadi Disember 2019 Bi Fatma amesema zaidi ya Shilingi Milioni mia mbili sabini na nane zimekusanywa

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!