MH. TABIA MAULID AMEAHIDI KUJENGWA NYUMBA YA KUINUA SANAA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR

Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo mh. Tabia maulid mwita ameahidi  kujengwa kwa nyumba  ya kuinua  sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini.{house  of talent zanzibar}

Akizungumza na wasanii wa chama cha muziki wa kizazi kipya rahaleo amesema hatua hiyo itasaidia kukuza vipaji vya wanamuziki na kutoa ajira kwa vijana.

Amesema atahakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha katika sanaa ya muziki ili iweze kukuwa na kuitangaza zanzibar kimuziki kupitia utekelezaji wa mipango mikakati mbali mbali ikiwemo kuboreshwa  kwa nyumba ya sanaa na wachezaji kupelekwa kushiriki matamasha ya kisanaa nje ya nchi.

 

Wakati huo huo mh. Tabia ameitumia fursa hiyo kuhamasisha fainali ya mechi za yamle yamle cup itakayochezwa siku ya jumamosi ya tarehe 12 mwezi huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa raisi wa zanzibar na mwenyekiti  wa baraza la mapinduzi dk. Hussein ali mwinyi.

 

Comments are closed.