MH.MAHMOUD AMEVIASA VYOMBO VYA HABARI KUCHUKUWA TAHADHARI YA KUTOVUNJA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale  Mh.Mahmoud Thabit Kombo ameviasa Vyombo vya Habari hasa  Redio kuchukuwa tahadhari ya kutovunja amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Akizungumza katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Redio Duniani  amesema zipo baadhi ya Redio katika kipindi hicho zinaamua kufungamana na Vyama vya Siasa lakini kinachohitajika kuzingatiwa misingi ya amani na utulivu ili kujenga Taifa lenye Umoja.

Mh.Kombo amefahamisha kuwa Redio ni moja ya Chombo muhimu na rahisi kufikisha Taarifa kwa Jamii haraka hivyo kinachohitajika kutayarishwa vipindi vinavyoweza  kuleta mabadiliko katika maisha yao ya kila.

Akitoa maelezo mafupi ya siku hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Redio za Kijamii Nd.Tadio Prosper Kwigize amesema katika kurahisisha dhana ya Redio kuwa jumuishi ni vyema Serikali kuwekwa mazingira ya kupunguza vikwazo vya Sera na Sheria ili Vyombo vya Habari vifanye kazi kwa ufanisi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii na Mmabo ya Kale anaesimamia Habari Nd.Saleh Yussuf Mnemo pamoja na baadhi ya Waandishi Waandamizi wamezungumzi umuhimu wa Redio kwa kuijenga Jamii na maendeleo ya Taifa.

Maadhimisho hayo ya siku ya Redio hufanyika kila Mwaka kukumbushia umuhimu wa Redio kwa maendelo ya Taifa ambapo kwa Mwaka huu yakiwa na Kauli mbiu ni Redio na Ujumuishaji.

Comments are closed.

error: Content is protected !!