MASHINDANO YA MPIRA WA MEZA YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YAMEZINDULIWA RASMI

Mashindano ya mpira wa meza ya afrika mashariki na kati chini ya umri wa miaka 18 yamezinduliwa rasmi kigali nchini rwanda ambapo zaidi ya mataifa 6 yameshiriki mashindano hayo.

akiyafungua mashindano hayo rais wa shirikisho la mpira wa meza nchini rwanda John Guruma amesema mashindano hayo yanatambuliwa na shirikisho la mpira wa meza dunia ittf ambapo washindi watawekwa kwenye rikodi ndani ya shirikisho hilo.

amesema mashindano hayo yatawapa nafasi kubwa nchi za ukanda wa afrika mashariki kupata uzowefu mkubwa wa kushiriki mashindano ya kimataifa.

No Comments Yet.

Leave a comment