Kamati ya fedha biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi imesema imefarijika kuanzishwa kwa kitengo cha kutoa huduma kwa wawekezaji na wafanyabiashara ili kurahisisha upatikanaji w huduma kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na mswada wa sheria ya kufuta sheria ya ukuzaji na kulinda vitega uchumi zanzibar amesema mswada huu umeletwa katika wakati muafaka ili kuendana na mageuzi ya kiuchumi kutoka wa kutegemea kilmo hadi uchumi wa viwanda kupitia wawekezaji tofauti.
Amesema kamati imeishauri wizara au taasisi zinazopaswa kushughulikia kitengo hicho kuwa na maofisa wenye uwezo wa kutoa maamuzi yenye maslahi kwa maendeleo ya uwekezaji nchini.
Wakichangia mswada huo wajumbe wa baraza hilo wamesema uwepo wa mswada huo utawezesha kuondokana na urasimu wa ufuatiliaji wa huduma katika ofisi mbalimbali kunakopelekea kuwavunja moyo wawekezaji kuwekeza miradi yao hapa nchini.