Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar inalenga kuhahakikisha kuwa kupanuka kwa huduma na ongezeko la ndege katika viwanja vyake ni kunaendana na uhakika wa usalama katika utoaji wa huduma.
Tamko hilo limetolewa na meneja wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume wakati akifungua mafunzo juu ya usalama wa viwanja vya ndege kwa watendaji wa idara mbali mbali yalioendeshwa na wakufunzi kutoka mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania .
Amesema lengo ni kuwatarisha wafanyakazi kutambua hatua za awali za matukio ya hatari katika viwanja vya ndege na kuweza kuchukua hatua zinazofaa na za kitaalamu katika kuzipatia ufumbuzi kulingana na kanuni za kimataifa.
Mkufunzi Benard Kavishe kutoka mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania amesema utoaji wa huduma katika viwanja vya ndege duniani unakabiliana na changamoto tofauti lakini zinaweza kuepukika iwapo watoaji wa huduma na wadau watakuwa wakijengewa uelewa wa kufahamu jinsi ya kuzitatua.
Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume umekuwa na ongezeko la ndege zinazotuwa kufuatia kuimarika kwa huduma kulikochangiwa na ujenzi wa bararara ya kuruka na kutua kwa ndege kiwanjani hapo,