MAKATIBU WAKUU WATAKIWA KUWAPA MASHIRIKIANO MAAFISA WA MFUMO WA SEMA NA RAIS MWINYI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed SuleimanAabdulla amewataka Makatibu Wakuu kuwapa mashirikiano Maafisa wa mfumo wa sema na Rais Mwinyi ili kusaidia kuyatolea ufumbuzi malalamiko ya Wananchi.

Mhe Hemed ametoa maelekezo hayo kupitia kikao maalum kilichowakutanisha Makatibu wakuu kilichojadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa sema na Rais Mwinyi alipokutana nao   Ofisini kwake Vuga jijini Zanzibar.

Amesema kutokana na Makatibu Wakuu kuwa Watendaji wa wizara ni vyema  kutoa mashirikiano yakutosha kwa kuwa karibu na maafisa walioteuliwa kusimamia mfumo huo ili kuwasaidia katika utendaji wao.

Aidha Mhe makamu wa Pili wa Raisi amewakumbusha watendaji hao  kuwa na kawaida ya kufatilia mfumo huo ili kujua  maoni na malalamiko ya Wananchi yanavyoelekezwa katika idara zilizo Chini ya Wizara zao.

Akielezea kuhusu mfumo huo  Mhe. Hemed ameeleza  kwamba

kwa upande  wake Katibu Mkuu Kiongozi naKkatibu wa Baraza la Mapinduzi Injinia Zena Ahmed said amesema  utoaji wa Taarifa kuhusu muendelezo wa utatuzi wa malalamiko ya Wananchi ni moja ya njia za kutatua changamoto hizo.

Ameeleza kuwa kuna haja kwa watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi kutoa mrejesho kwa Wananchi juu ya changamoto wanazoziwasilisha kwani kufanya hivyo kutajenga imani kwa Wananchi juu ya Serikali yao inayongozwa na Rais Dk. Mwinyi.

Wakichangia mada katika kikao hicho makatibu wakuu  wamemuahidi Makamu wa pili wa Rais kwamba  watashirikiana vyema na wakuu wa Taasisi katika kuwasimamia maafisa wa mfumo huo kwa  kufahamu changamoto zao ili kutumia muda mfupi katika kuyatolea ufafanuzi malalamiko ya Wananchi.

Mapema makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alikutana na kufanya mazungumzo na maafisa wasimamizi wa mfumo huo kutoka katika idara mbali mbali na kuwataka wakasimamie vyema majukumu yao bila ya woga.

Kupitia kikao hicho maafisa hao wamemeueleza makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar kuwa mfumo huo ni mzuri hasa kwa kuweza kuisadia Serikali katika kufahamu yaliyomo katika jamii na hata katika maeneo ya kazi pamoja na kuanisha baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo kukosekana kwa Rasilimali fedha kwa ajili ya kukidhi haja ya mawasiliano.

 

 

Comments are closed.