MAJINA NANE YA WAJUMBE WA KAMATI YA UHAMASISHAJI WAKATI WA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI CUP

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Omar Hassan Kingi ametangaza Majina Nane ya Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji wakati wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup.

Kamati hiyo itakayojumuisha Wajumbe kutoka Zanzibar na Tanzania Bara itaongozwa na Mwenyekiti Taufiq Salim Tturkey ambae ni mbunge wa Jimbo la Mpendae na Wajumbe wengine saba ambao ni Hassan Mussa Ibrahim (Has T), Salum Issa Ameir, Mwanahawa Rajab Iddi, Khamis Mwinjuma (Mwana Fa) Jeri Muro,  Salama Jabir na Ali Saleh (Albato).

Akitangaza Majina hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Tabia Maulid Mwita amesema lengo la Kamati hiyo ni kunogesha  na kuwahamasisha Wananchi kupitia Wasanii wa Sanaa za Asili, Maigizo na kizazi  kipya ili kuwezesha kufana kwa Sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha amesema Kamati hiyo itakuwa na Majukumu ya kuratibu na kusimamia Wasanii pamoja na upatikanaji wa Fedha kutoka kwa Wadau wa michezo, Wafadhili na Taasisi Binafsi kwa ajili ya uendeshaji wa Michuano hiyo.

Kingi pia ameitumia fursa hiyo kuwashajihisha Wananchi kushiriki kwa wingi katika Michuano hiyo yenye mnasaba wa kuyaenzi   Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Hamasa za Wasanii mbali mbali zitatumbuizwa kabla ya  Mechi, wakati wa mapumziko na baada ya Mechi.

 

Comments are closed.