MADALALI WA SAMAKI SOKO LA KIHINANI KUCHUKULIWA HATUA

Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi imesema itawachukulia hatua za kisheria baadhi ya Madalali wa Samaki katika Soko la Kihinani ambao hawachukui tahadhari dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkuu wa Mkoa  huo  Mhe. Hassan Khatib  Hassan ameeeleza hayo wakati wa ziara katika eneo la Mnada huo akiwa pamoja na Viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Magharibi ‘a’, kuangalia utekelezaji wa hatua zinazochukuliwa na Wafanyabiashara hao kuhusu Kujikinga ya Maradhi hayo.

Amesema licha ya hatua zinazochukuliwa na Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa bado kuna baadhi ya Watu wanakwenda kinyume na maelekezo hayo.

Viongozi wa Mnada wa Soko la Samaki la Kihinani wamesema wataendelelea kushirikiana na Serikali kusimamia maelekezo na Maagizo yalitotolewa ikiwemo kutumia Vifaa Kinga na kutoa Elimu ya Kujikinga kwa Wafanyabiashara na wateja katika Eneo hilo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharibi ‘a’ Amour Ali Mussa amesema  hatua mbali mbali wamechukua ya kukutana na makundi  tofauti na  kuwapatia Elimu ya  kujikinga na Virusi vya Corona lakini muitikio bado  unaonekana ni mdogo.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!