KUTOA MAELEZO SAHIHI YA MATUMIZI YA MADAWA YA ANTIBIOTIC

Waziri wa afya mhe: hamad rashid mohamed  amewataka  wadau wa sekta ya afya  ya wanadamu na mifugo   kutoa maelezo sahihi ya matumizi ya madawa ya antibiotic    ili kuzuiya usugu wa vimelea unaosababishwa na matumizi mabaya ya  madawa .

Akifunguwa kikao    cha   utengenezaji wa nyaraka    ambazo   zitakuwa   muongozo   juu ya  udhibiti    wa matumizi mabaya ya madawa kwa binadamu na wanyama   kilichofanyika  katika  hotel ya ocean view  huko kilimani  ambao uliwashirikisha wadau kutoka katika taasisi mbali mbali  hapa nchini.

Amesema madhara y a utumiaji wa madawa kiholela ni makubwa kwa wanadamu  na mifugo   hivyo  ni muhimu kwa wataalamu kujadili kwa kina suala hili pia kutoa  elimu kwa wananchi  kuwacha kutumia madawa kiholele  bila ya maelekezo kutoka  kwa madaktari  husika  na kuweza kusaidia  jamii ambayo ndio nguvu kazi ya taifa .

Akiwasilisha mada katika kikao hicho muwakilishi kutoka  shirika  la kilimo  na  chakula   dr.bachana rubengwa  amesema tatizo la matumizi mabaya ya dawa lipo na kwa upande wa tanzania bara wameshakaa pamoja na kuandaa mpango kazi ambao unasimamiwa na  shirika  hilo pamoja na kusaidia kutoa elimu kwa jamii, vifaa katika maabara pamoja na tafiti  ambazo zitaonesha ukubwa wa tatizo hilo kwa ujumla wake.

Akieleza malengo ya mpango   huo  dr.khadija nuor omar  amesema  ni muhimu  kuwa na mpango  utakao tekelezwa kwa upande  wa zanzibar  kwakuwa tafiti zinaonesha kuwepo kwa matumizi ya  antibotic kiholela   hiyo jitihada za makusudi zinaendelea kuchukuliwa na kuweza kupata  matokeo yake.

Kikao hicho cha siku 5 kimefadhiliwa na shirika la kilimo n a chakula fao

 

 

Comments are closed.