KONGAMANO KUHUSU UCHUMI WA BLUU

Jaji Mkuu wa Zanzibar mh.Omar Othman Makungu amewataka Waislamu kuzingatia matumizi sahihi ya raslimali za Bahari ili kuona zinaendelea kuwa chanzo kikuu katika kukuza uchumi wao

Akifungua Kongamano la Mwezi mtukufu wa Ramadhani kuhusiana na Uchumi wa Blue huko Mahonda amesema bado baadhi ya wanajamii wanaendelea kufanya shughuli za Bahari pasipo kuzingatia umuhimu wa matumizi bora na hatimae kusababisha viumbe Bahari kupungua upatikanaji wake.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Kongamano hilo limetoa fursa kwa wakaazi wa Mkoa huo kuona uwezo na vipaji vyao kidini pamoja na kujifunza kuendeleza tamaduni za Kiislamu ikiwemo utowaji wa Zaka na Sadaka.

Akitoa taarifa fupi ya Kongamano hilo kupitia Taasisi ya kusaidia jamii Zanzibar Relief and Development Foundation (Zardefo) Katibu mkuu wa taasisi hiyo Ali Mohammed Haji, amesema Kongamano hilo lina lengo la kuwakumbusha Waislam mambo muhimu kuhusiana na dini yao pamoja na umuhimu wa Uchumi wa blue katika Uislamu.

Wakiwasilisha mada ya Uchumi wa buluu katika Uislamu Sheikh Izuddin Alawi na Sheikh Mubarak Awesu wamempongeza Rais wa Zanzibar kwa wazo lake hilo pamoja na kumuombea dua katika kuhakikisha anaibadilisha Zanzibar kupitia Uchumi huo.

Comments are closed.