KIKAO CHA LA WAWAKILISHI KIMEENDELEA

Serikali imesema kuongezeka kwa taka za plastiki katika maeneo ya Bahari kumesababishwa na kuzagaa kwa taka katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini.

Akijibu  swali katika Baraza la Wawakilishi kuhusu hatua za Serikali za kudhibiti taka Baharini Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais   Mihayo Juma Nh’unga amesema Serikali inaendelea na juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kujenga Jaa la kisasa la Kibele na kuandaa mkakati wa Kitaifa wa usimamizi wa taka

Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amesema Serikali inawalinda wawekezaji Nchini kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa  Nchini .

Ameeleza hayo wakati akijibu maswali katika Baraza la Wawakilishi juu ya kuwalinda na kuwatetea wawekezaji Nchini ambapo amesema licha ya haki hiyo ya ulinzi lakini pia Wawekezaji hao nao wana wajibu wa kutii Sheria na Masharti yauwekezaji yaliyowekwa.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!