JUMUIYA YA MUZDALIFA IMEISAIDIA WIZARA YA ELIMU PRINTA 130

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma Amesema si busara kwa Walimu kuvujisha mitihani kwa Wanafunzi kwani vitendo hivyo vinashusha hadhi ya Elimu Nchini.

Amesema katika kudhibiti hali hiyo wanapaswa kuendelea kushirikiana na Walimu Wakuu ili kusimamia pamoja na kuweka mikakati bora ya kuondosha vitendo hivyo ikiwemo ufuatiliaji wa Masomo kwa Wanafunzi.

Akizungumza baada kupokea msaada wa Printa 130 kutoka Jumuiya ya Muzdalfa, Mhe. Riziki ameishukuru Taasisi hiyo  kwa kusaidia ukuaji wa Sekta ya Elimu Zanzibar na kusema hatua hiyo italeta mageuzi katika utendaji wa kazi za Skuli.

Mwenyekiti  wa Muzdalifa Nd. Abdalla Hadhar Abdalla amesema wametoa vifaa hivyo kuondosha matatizo yanayozikabili Skuli mbali mbali ya kutumia Ofisi za Nje kwa kazi zao kitendo ambacho kinasababisha kuvuja kwa baadhi ya siri ikiwemo mitihani.

Zaidi ya Shillingi Millioni 34 zimetumika kwa ununuzi wa Vifaa hivyo.

Comments are closed.

error: Content is protected !!