JUMLA YA WAGONJWA 12 WAMETHIBITISHWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA CORONA NCHINI TANZANIA HADI SASA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Wasafiri wanaotoka katika Nchi zenye Maambukizi ya Virusi vya Corona wanaokuja Tanzania watawekwa katika Karantini ya Siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

Akilihutubia Taifa amesema hadi sasa Wagonjwa 12 wamethibitika kuambukizwa na Ugonjwa huo wakiwemo Raia wa Kigeni na Watanzania.

Rais Magufuli amefahamisha kuwa Wagonjwa wote wanaendelea vizuri na hadi sasa hakuna Kifo na vipimo 20 vya leo vilivyochukuliwa hakuna Mtu aliyekutwa na Maambukizi ambapo pia Mgonjwa wa kwanza aliyeripotiwa kupata Ugonjwa wa Corona   Tanzania ameshapona.

Kwa mujibu wa Takwimu tayari Ugonjwa wa Homa ya Corona umewakumba  Watu zaidi ya Laki Mbili na Elfu 60 katika Nchi zaidi ya 160 Duniani,  na hadi sasa kiasi Watu elfu 11, wamepoteza maisha.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!