JUMLA YA MADAWATI 4,545 YANATARAJIWA KUGAIWA KWA SKULI ZA UNGUJA NA PEMBA

Kamati  ya Kitaifa  ya  Madawati  Zanzibar inatarajia kugawa Madawati  4,545  kwa Skuli za Msingi  za Unguja na Pemba kwa awamu ya kwanza ili kupunguza uhaba wa Madawati  kwa Wanafunzi .

Akiyakagua Madawati hayo ikiwa ni mchango wa Wadau mbali mbali Mwenyekiti wa Kamti hiyo Mh Haroun Ali Suleiman amesema  hatua hiyo ni miongoni mwa Juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein za kuhakikisha tatizo la uhaba wa Madawati  kwa Wanafunzi  linamalizika.

Mh Haroun amezitaka  Skuli zitazobahatika kupata Madawati hayo kundaa Kamati za kusimamia  utunzaji  ili yaweze kudumu kwa muda mrefu .

Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Nd .Khalid Masoud Waziri amesema Madawati hayo ya Awamu ya Kwanza yameletwa Kontena tisa ambapo Awamu ya Pili yanatarajiwa kuletwa Kontena kumi na tatu na yalitarajiwa kufika hivi karibuni lakini yamechelewa kutokana na Mripuko wa Janga la maradhi ya Korona iliyoikumba Dunia .

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Simai Mohammed Said ameielezea kazi  inayofanywa na Kamati  hiyo  kuwa  ya Kizalendo  na imefanywa  kwa  wakati  muafaka  hatua  itakayochamgia  kasi  ya  ukuaji  wa  Sekta  ya  Elimu.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!