JESHI LA NIGER LAUA MAGAIDI 38 WA BOKO HARAM KATIKA MAPIGANO MAKALI

Wizara ya ulinzi wa niger imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limewauwa magaidi 38 wa kundi la boko haram katika mapigano makali yaliyojiri kusini mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa magaidi hao wa boko haram walikuwa na idadi kubwa ya silaha wakati waliposhambulia kituo cha jeshi karibu na gueskerou katika eneo la diffa. Boko haram ni kundi lenye misimamo ya kuvuka mipaka ambalo chimbuko lake ni kaskazini mwa nigeria. Kundi hilo la magaidi limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji pamoja na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo. Magaidi wa boko haram wameeneza ugaidi wao katika nchi jirani za niger na cameroon.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!