JAMII NA KUWEZA KUWACHAGUA WANAWAKE KATIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Tamwa kwa upande wa Zanzibar kimeridhia Ripoti ya taarifa iliyotolewa na Wanaharakati, Wanaume wa mabadiliko pamoja na Viongozi wa dini kuhusu kuhamasisha Wanawake kushika nafasi mbalimbali  za Uongozi kupitia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Akizungumzakatika uwasilishaji wa Ripoti hiyo Afisa miradi kutoka TAMWA nd. sabrina  yussuf amesema mafanikio hayo yameweza  kupiga hatua kwa jamii na kuweza kuwachagua wanawake katika nafasi mbalimbali ya uongozi.

Hata hivyo amezipongeza kamati hizo kwa  juhudi zao za kuelimisha jamii mjini na vijijini kwa vile kuna baadhi ya mambo yanahitajika kusemewa na wanawake wenyewe katika vyombo vya kutunga sheria.

Nao wanaume haowa mabadiliko wakielezea namna harakati hizo zilivyofanikiwa wamesema wamefanikiwa kuondosha mfumo dume uliozoeleka ndani ya jamii ya kuwa mwanamke hana uwezo wa kuongoza.

Comments are closed.