IDARA YA UHAMIAJI KUENDELEA KUWAJIBIKA NA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Mohammed Aboud Mohammed ameitaka idara ya uhamiaji kuendelea  kuwajibika na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuilinda zanzibar na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza katika hafla ya kuagwa wastaafu wa idara ya uhamiaji Zanzibar waliostaafu mwaka 2019 katika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul Wakil amesema kuendelea kufanya hivyo kutapunguza mianya ya wahalifu

Mhe. Aboud akitoa nasaha zake kwa wastaafu hao ameeleza kuwa katika safari ya utumishi wa umma hakuna ugumu katika maisha mapya jambo la msingi ni kumtanguliza mungu.

Kamishna wa uhamiaji zanzibar nd. Johari Sururu amewasisitiza wastaafu hao    kujumuika  vizuri na jamii pamoja na familia zao na kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii.

Akisoma risala ya wastaafu naibu kamishna mstaafu Ali Suleiman Nassor ameishukuru idara ya uhamiaji kwa mashirikiano waliyoyapata na amesisitiza kufanya kazi kwa nidhamu kwani bila ya nidhamu hakutakuwa na ufanisi katika utendaji

Comments are closed.

error: Content is protected !!