DR.SHEIN AWATAKA WATENDAJI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewataka watendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar kufanya kazi kwa mujibu wa misingi ya Serikali na ushirikiano ili kuhakikisha shirika hilo linafikia malengo ya kuanzishwa kwake.

Akizungumza na watendaji wa shirika hilo kwa upande wa Televisheni amesema ni lazima watendaji hao kufuata taratibu na kuacha tabia ya kupendelea vikundi au baadhi ya watu katika kufanya kazi zao.

Rais Shein  amefahamisha kuwa kutasaidia kuliondosha shirika hilo katika mfumo wa kizamani sambamba na kuliendeleza na kuweze kujitegemea kwa muda mfupi.

Ameeleza kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuliimarisha shirika hilo huku akisistiza kwa uongozi wa ZBC Wizara kukaa pamoja na uongozi wa  wizara ya habari utalii na mambo ya kale kupanga vipaumbele katika kutatua changamoto zinazozikabili shirika hilo kwa sasa

Aidha ameliagiza shirika laZBCkuhakisha wanafanya utaratibu wa kuwasilisha maombi serikalini kwa ajili ya wafanyakazi wa kujitolea waweze kuajiriwa mara moja

Katibu mkuu kiongozi dk Abdulhamid Yahya Mzee ametolea uafafanuzi wa baadhi ya matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa Shirika hilo ikiwemo kuimarishwa kwa .maslahi yao

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC nd Chande Omar amesema kwa sasa shirika hilo lipo katika hatua za kuungnisha studio ya Radio va TV ili kurahisisha matangazo .

Baadhi ya wafanyakazi waliopata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine wamemuomba mh  rais kulisimamia suala la upatikanaji wa gari la matangazo ya nje ya studio  ob van na mafunzo ya kuimarisha kazi zao.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!