DKT MAGUFULI AMEAHIDI KUJENGA UWANJA MKUBWA WA KISASA WA MICHEZO DODOMA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa kisasa wa Michezo utakaokwenda sambamba na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.

Akizungumza katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma amesema hatua hiyo na nyenginezo zinalenga kuimarisha zaidi Jiji la Dodoma.

Dkt Magufuli amesema Watanzania wanataka mabadiliko katika Sekta mbali mbali jambo ambalo linatekelezwa katika hatua tofati.

Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kulinda Rasilimali za Madini, kupambana na Rushwa Ununuzi wa Ndege Mpya 11 na kurejesha nidhamu kwa watendaji wa Umma.

Aidha ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa Ndege Mjini Dodoma utakaokuwa na uwezo wa kusafirisha Abiria moja kwa moja kuelekea Nchi za Nje.

Sambamba na hayo amesema Serikali itanunua Ndege nyengine mpya Tano ikiwemo ya kubebea Mizigo.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ali akitoa muhutasari wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 amesema inalenga kuhimiza Wananchi kuwa Wazalendo kwa Nchi yao na kutunza Rasilimali za Taifa ziwe chachu ya Maendeleo.

Amesema ataendelea kuilinda Amani na Mapinduzi ya Zanzibar ili kuimarisha maendeleo ya Tanzania.

Comments are closed.

error: Content is protected !!