DK.MAGUFULI AMEWATAKA WATANZANIA KUPUNGUZA HOFU JUU YA JANGA LA UGONJWA WA HOMA YA CORONA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Amewataka Watanzania kupunguza hofu juu ya Janga la Ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona na badala yake waendelee kufanya kazi na kujenga Uchumi kwa kuzingatia tahadhari zote za kujikinga.

Rais Magufuli ameeleza hayo katika Salamu zake za Ibada ya Jumapili Mjini Dodoma ambapo amesema kuwepo kwa Ugonjwa wa Corona isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mwenyezi Mungu, na kutoa Wito kwa Watanzania wote Kumuomba Mwenyezi Mungu ili aliepusha Janga hili.

Rais Magufuli amekemea tabia za baadhi ya Watu wanaofanya Mzaha juu ya Ugonjwa huu ama kuwatia hofu Wananchi kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii, na badala yake ametaka Watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakingatia tahadhari zinazotolewa na Wataalamu.

Aidha amewashukuru Viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha Wananchi kuchukua tahadhari na ametoa Wito kwa Viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aepushe Janga hili la Corona.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!