Vijana Wametakiwa kuthamini Michezo kwani imekuwa ni Ajira ya Kudumu ambayo inaweza kubadilisha Maisha kwa kuwaingizia Kipato.
Akizungumza katika Mashindano ya Yamle Yamle katika Uwanja wa Magirisi Meli Nne Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi amesema Vijana wanawezo Mkubwa wa kujiajiri kupitia Sekta ya Michezo ambayo imekuwa ikiimarika Duniani kote.
Nae Mratibu wa Mashindano hayo Nd.Jecha Simai Jecha Amesema wapo katika hatua za Mwisho kumaliza Makundi huku Akipongeza ujio wa Dk.Mwinyi katika Mashindano hayo ambapo Mchezo wa Leo Timu ya Taifa Tangini Kutoka Bwejuu wamefanikiwa kuifunga Timu ya Anfiled ya Bububu Bao 1-0 .