DK HUSSEIN MWINYI AMETOA MUDA WA MIEZI MITATU KUKAMILISHWA KWA MIRADI YOTE YA HUDUMA ZA MJINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ametoa muda wa miezi mitatu kukamilishwa kwa Miradi yote ya kuimarisha Huduma za Mjini ikiwemo ujenzi na Usafi wa Mitaro

Akizungumza katika Ziara ya kukagua hatua zilizofikiwa juu ya Miradi ya kuweka Mji safi amesema  kumekuwa na kiwango kikubwa cha uchafu hali inayoharibu haiba ya Jiji la  Zanzibar

Dk Mwinyi amefahamisha kumekuwa na Miradi iliyoanzishwa kwa ajili ya kuimarisha Miji iliyogharimu Fedha nyingi lakini hadi sasa ukamilishaji wake umekuwa hauzingatii muda uliopangwa hali ambayo inaharibu malengo ya Serikali katika kupambana na uchafu katika Maeneo yote.

Aidha ameiagiza Wizara ya fedha kuacha kusimamia Miradi inayoendeshwa na Taasisi mbali mbali ikiwemo Manispaa na badala yake waombe Mikopo kupitia benki mbali mbali ambapo utekelezaji wa Miradi hiyo iachiwe mamlaka husika kwani wao ndio wenye utaalamu wa kutekeleza na kufahamu mahitaji halisi

Kufuatia Ziara hiyo Mh Rais pia ameagiza watendaji hao kuhakikisha barabara ya kuanzia Uwanja wa Ndege hadi hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa na muonekano mwengine ikiwemo kuimarisha Bustani na Usafi ili kuwa kivutio kwa Wageni

Dk Mwinyi pia ameyaagiza mabaraza ya Manispaa Mjini, Magharib A na B kuliondosha Jaa la Amani pamoja na kusafisha mitaro na kutokutekelezwa kwake hakutakuwa na haja ya kuwaacha katika nafasi za Uongongozi

Nae Msimamizi wa Mradi wa kuimarisha huduma za jamii mjini zusp bw makame ali amesema Mradi huo uliwashirikisha Wahandisi kutoka Manispaa zote za Mji licha ya kuwepo kasoro katika utekelezaji wake

Ziara hiyo ya Dk Hussein Mwinyi imeanzia Uwanja wa Ndege Kilimani, hadi kituo cha kukusanyia Taka Maruhubi ,Jaa la Amani jaa la kisasa kibele na kumalizia  Kwarara.

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!