DK.ALI MOHAMED SHEIN ANATARJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADDHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein anatarjiwa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar .

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu amesema maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na uwekekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Mahakama Kuu liliopo Tunguu.

Amesema mbali na uwekaji wa jiwe la msingi pia kutakuwa na maonesho ya mambo ya sheria ambayo yatafanyika katika Viwanja vya Maisara kuanzia febuari 7 ambapo taasisi zinazosimamia masuala ya sheria zitashiriki na kuweza kutoa elimu kwa Wananchi.

Jaji Makungu amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni dumisha utawala wa sheria na demokrasia katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo kauli mbiu hiyo itaenda sambamba na kuelekea uchaguzi  katika kudumisha Amani.

Aidha Mh. Makungu amewataka Wananchi kushiriki kwa wingi katika maonesho hayo ili kuweza kupata ufahamu juu ya masuala ya sheria na kuweza kupatiwa ufumbuzi katika mambo mbali mbali.

Comments are closed.

error: Content is protected !!