DHAMIRA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NI KUHAKIKISHA KILA MWANANCHI ANAPATA HUDUMA BORA

Naibu waziri wizara ya afya Mhe Harous Said Suleiman amesema dhamira ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya popote alipo ili kuhakikisha jamii inakuwa na afya bora.

Naibu waziri wa afya amesema hayo wakati akifungua mafunzo maalum ya kuelimisha jamii juu ya maradhi mbali mbali ikiwemo kichocho ,malaria na ukimwi yanayoendeshwa na ngo ya chiwahili chini ya madaktari bingwa kutoka china yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za ngo hiyo huko kijichi wilaya ya mghrib a.

Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar inathamini michango inayotolewa  kutoka china katika nyanja mbali ikiwemo kuimarisha afya  za wananchi wa zanzibar kupitia sekta ya afya.

Prof Li Xianyi amesema  taasisi ya ccuc pia inawasadia vijana katika masuala ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa huduma ya afya ya elimu ya kujikinga na maradhi mbali mbali ndani ya jamii kupitia madaktari wa kujitolea.

Baadhi ya  washiriki wa mafunzo  hayo  kutoka wilaya mbali za unguja  wamesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yatawasaidia kufika elimu hiyo katika taasisi zao wanazotoka.

No Comments Yet.

Leave a comment

error: Content is protected !!