CORONA IMESABABISHA KUSHUKA KWA BEI YA SAMAKI ZANZIBAR

Kumekuwa na Kiwango kikubwa cha kushuka kwa Bei ya Samaki katika Diko la Kihinani Ngalawa kufuatia kufungwa kwa Hoteli nyingi za Kitalii kufuatia maambukizi ya Virusi vya Corona.

Licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya Samaki wanaovuliwa kwa Siku ZBC imebaini kuwa baadhi ya Wavuvi wameamua kusimamisha Shughuli zao kuepuka Misongamano ndani ya Vyombo wanapokwenda wanapoenda kuvua.

Shaaban Juma Khamis Mkuu wa Diko la Ngalawa Kihinani ameiambia ZBC kuwa Awali Diko hilo limekuwa likipokea kilo Elfu Tano kwa Siku na sasa imeshuka hadi  kilo Elfu Mbili.

Baadhi ya Wafanyabiashara wa Samaki ambao wengine walikuwa wakipeleka Samaki Hotelini na kuchuuza Mitaani wamesema kushuka kwa Bei ya Samaki kunatokana na kuzorota kwa Shughuli za Kitalii hapa Zanzibar.

Mbali na Soko la Kihinani Ngalawa  ZBC  pia ilitembelea Diko la Mazizini na Kizingo ambapo ndani ya Madiko hayo utaratibu wa Kujikinga na Mripuko wa Maradhi ya Corona kama ulivyoagizwa na Serikali umezingatiwa.

Comments are closed.