Category Archives: Michezo na Burudani

WANANCHI WAMETAKIWA KUTUNZA NA KUENZI UTAMADUNI

Wananchi wametakiwa kutunza utamaduni  na kuenzi  kwani ndio unaokusanya na kuleta  vivutio mbalimbali   vya utalii ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ufungaji wa tamsha la mtanzania  katika ukumbi wa ngome kpngwe Mh Naibu Waziri wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mh Mohammed Ahmada Salim amesema  matamasha kama haya yanakuza utalii ikiwemo na utamaduni  ndio unaokusanya watu mbalimbali na vivutio viliopo ndani ya z’bar .

Hata hivyo amesisitiza kuwa utalii ni uti wa mgongo katika visiwa vya z’bar  kwani kiasi cha shilingi milioni 5 zimeweza  kupokelewa kutokana na utalii.

Tamasha hilo la pili ambalo  limepambwa kikundi cha modem taarab,pamoja na michezo mbalimbali ya bao na mchezo wa draft. Ambayo ilisisimua hisia za wananchi waliofika katika eneo hilo.

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR KUTINGA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA CECAFA

Timu ya taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 20 karume boys imefufuwa matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya CECAFA kagame cup inayoendelea mjini jinja nchin uganda.

Ndani ya dimba la njeru mjini jinja vijana hao wa karume boys wamefufuwa matumaini ya kuingia robo fainali katika michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya ethiopia.

Bao la kwanza limefungwa na sadam makame katika dakika ya 17 dominic kasco haga dakika za lala salama ya 88. Kwa upande wa goli pekee la ethiopia limefungwa na  adebayo huu hajiso kipindi cha kwanza dakika ya 48.

Mwalim msaidizi wa kikosi cha karume boys Ibrahim Moh’d Makeresa pamoja na naodha wa wa timu hiyo wamese imilikuwa sio rahisi kuifunga ethiopia ukilinganisha na imara timu hiyo.

Mchezo mwengine karume boys watacheza kesho majira ya saa kumi jioni dhidi ya ndugu zao wa tanzania bara ngororo katika kiwanja cha njeru mjini jinja

SHILINGI MILIONI 10 ZAGAIWA KWA TIMU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU YA WATU WENYE ULEMAVU

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa shilingi milioni 10 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya  watu wenye ulemavu inayojiandaa kushiriki mashindano ya afrika   kuanza tarehe 01 mwezi ujao, mwaka huu nchini angola.

Katibu wa rais, wa Tanzania  ngusa samike amekabidhi fedha hizo kwa viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika hafla iliyofanyika studio za shirika la utangazaji tbc.

Wamesema timu hiyo yenye wachezaji 13, walimu 5 na viongozi 2 itaondoka tarehe 28 mwezi huu,  kuelekea nchini angola ambako inakwenda kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza huku wakiahidi kufanya vizuri.

WAWAKILISHI WA ZANZIBAR KWENYE MASHINDANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Malindi wameanza vibaya nyumbani baada ya kukubali kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Almasry ya Misri mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.

Mabao ya Almasry yamefungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27, 39, Hassan Ibrahim dakika ya 32 na Saidou Simpore dakika ya 52 huku bao pekee la Malindi likifungwa na Ibrahim Ali (Imu Mkoko) dakika ya 42.

Mchezo wa marudiano utachezwa Septemba 29, 2019 huko Misri ambapo Malindi anatakiwa kushinda 4-0 ugenini ndipo asonge mbele.