Category Archives: Michezo na Burudani

DK. HUSSEIN MWINYI AMEWATAKA VIJANA NCHINI KUTHAMINI MICHEZO KWA KUWEZA KUJIAJIRI KUPITIA SEKTA HIO

Vijana Wametakiwa kuthamini Michezo kwani imekuwa ni Ajira ya Kudumu ambayo inaweza kubadilisha Maisha kwa kuwaingizia Kipato.

Akizungumza katika Mashindano ya Yamle Yamle katika Uwanja wa Magirisi Meli Nne Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi amesema Vijana wanawezo Mkubwa wa kujiajiri kupitia Sekta ya Michezo ambayo imekuwa ikiimarika Duniani kote.

Nae Mratibu wa Mashindano hayo Nd.Jecha Simai Jecha Amesema wapo katika hatua za Mwisho kumaliza Makundi huku Akipongeza ujio wa Dk.Mwinyi katika Mashindano hayo ambapo Mchezo wa Leo  Timu ya Taifa Tangini Kutoka Bwejuu wamefanikiwa kuifunga Timu ya Anfiled ya Bububu Bao 1-0 .

WASANII WA TASNIA YA FILAMU NCHINI WAMETAKIWA KUJIONGEZA KITAALUMA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo   Nd.Amour Hamil Bakar Amewasisitiza Wasanii wa Tasnia ya Filamu Zanzibar kujiongeza Kitaaluma ili wapate fursa za kujifunza zaidi nafasi inapotokezea.

Akifunga Mafunzo ya Siku Kumi ya kuwajengea uwezo Wasanii Waandaaji wa Filamu pamoja na Waandishi wa Filamu Zanzibar Naibu Katibu Mkuu huyo Amesema Zanzibar ina Fursa ya kuwa na Wasanii wenye Uwezo wa kuzalisha Filamu zenye Viwango, ila kinacho wakwamisha ni uhaba wa Taaluma ya Tasnia hiyo.

Msimamizi na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Cosoza Zanzibar Ndugu Mtumwa Khatib Ameir, Amesema endapo Wasanii hao  wataitumia Taaluma walioipata katika Mafunzo hayo ya Siku 10 itawasaidia kukuza kipato cha Wasanii hao.

Wakufunzi wa Mafunzo hayo wamesema kazi za Wasanii hao zinaweza kuwa za Kimataifa iwapo Watapata Mafunzo ya ziada katika masuala ya Taa, Uungaji Picha na Sauti.

Washiriki wa Mafunzo hayo wameipongeza Taasisi ya Cosoza pamoja Wakufunzi wa Mafunzo hayo na kusema kuwa ni imani yao kuwa Mafunzo waliopatiwa, yamewaongezea Ujuzi zaidi na ni Matumaini yao kuwa Watafanya kazi zenye Ubora wa hali ya juu.

 

 

TIMU YA JKU ACADEMY IMEIFUNGA TIMU YA TAVETA CITY MABAO 5-2 KWENYE MASHINDANO YA YAMLE YAMLE

Timu ya JKU Academy imefanikiwa kupata alama tatu baada ya kuifunga timu ya TAVETA City mabao 5-2 kwenye mashindano ya Yamle Yamle mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Magirisi.

Vijana wa JKU Academy waliovalia Jezi Rangi nyekundu walionekanwa kuutawala Mchezo huo na kufanikiwa kupata mabao hayo 5 yaliyofungwa na Ahmed Khamis dk 36, Ramadhan Manzil dk 40, Mudrid Shehe dk 75 na Abubakar Hassan dk 50 na 80 huku mabao 2 ya Taveta cCty yakifungwa na Ali Haji dk 24 na Abrahman Juma dk 55.

Nahodha wa JKU Academy Abubakar Hassan amezungumzia siri ya ushindi wao.

Kwa upande wake Nahodha wa Taveta Mohd Iddi Duchi amesema walizidiwa na vijana wa JKU kutokana na kuwa pamoja muda mwingi kuliko wao wanaojuwana Uwanjani tu.

 

TIMU YA AUTO BRAZIL IMETOKA SARE YA BAO 1-1 DHIDI YA BANGALOO FC YA MAKUNDUCHI

Timu ya  Auto Brazil wamedhidi jiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika hatua ya 32 bora baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Bangaloo FC ya Makunduchi katika michuano ya Yamle Yamle yanayoendelea ndani ya Dimba la Magirisi arena .

Auto Brazil waliovalia Jezi rangi ya Manjano wamekubali kutoka sare katika Mchezo huo ambao uliokuwa wa kuvutia katika muda wote wa Mchezo.

Makocha wa Timu hizo wamesema Michuano hiyo imezidi kuwa mingumu hasa katika kuielekea ya 32 bora.

Wakati Mashabiki wanaofika Kiwanjani hapo wamejigamba kwa Timu zo kuzidi kufanya vizuri katika Michuano hiyo.

 

error: Content is protected !!