Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

CCM MKOA WA KASKAZINI IMESEMA HAKITAWATETEA WABUNGE NA WAWAKILISHI WASIOTIMIZA AHADI WALIZOZITOA

 

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja kimesema hakitawatetea Wabunge na Wawakilishi wasiotimiza ahadi walizozitoa walipokuwa wakiomba kura kwa Wananchi ndani ya Majimbo yao kwa vile wameshindwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi

Akizunguza katika Ziara ya Jimbo la Mkwajuni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa huo Idd Ali Ame Amesema Viongozi wote wa  CCM wanatekeleza ilani ya Chama kivitendo hivyo wale wasiowajibika Chama hakitompa ridhaa kurudi tena Jimbo.

Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni Mhe Ussi Yahya Amesema ndani ya Jimbo hilo wamefanikiwa kutatua kero za Wananchi kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma ya maji safi na salama tatizo lililokuwa likiwasumbua kwa muda mrefu.

Viongozi wa Jimbo hilo wamesema wanashirikiana kwa karibu sana na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo hilo kutatua kero za Wananchi pamoja na kuwashirikisha Wananchi ili kuleta maendeleo katika Jimbo lao.

 

WAZAZI PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAMEPONGEZA HUDUMA BORA WANAZOPATIWA NA MADAKTARI

Wazazi na Walezi wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wametakiwa kuwatunza watoto hao sambamba na kuwafikisha katika Clinic mpya ya watu wenye ulemavu huo ili waweze kupata kinga na tiba dhidi ya magonjwa mbali mbali.

Daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi Dk Hafidh Sheha Hasan ameeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo ulioambatana na utoaji wa elimu kwa watu wenye maradhi ya ngozi juu ya kujikinga na magonjwa ya saratani ikiwa inakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.

Amesema watu wenye ulemavu wanahaki ya kupata elimu ya kujikinga na mionzi ya jua kwani inaweza kusababisha athari za ngozi pamja na uoni wao.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk Jamal Adam Taib kuanzishwa kwa Clinik hiyo ni ishara ya kutekeza mikakati iliyowekwa na Serikali katika kuhakikisha huduma bora za Afya zinapatikana kwa kila mtu ndani ya hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wa ngozi  Zanzibar amesifu jitihada za Serikali kwa kutatua changamoto ambayo iliwakabili kwa muda mrefu.

Baadhi ya Wazazi pamoja na Watoto wenye ulemavu wa ngozi  wamepongeza huduma bora wanazopatiwa  na Madaktari pamoja na Jumuiya ya Tumaini ambayo ndio msaada mkubwa kwao kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

WANANCHI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NA MASHIRIKA KATIKA KUPIGA VITA MARADHI YA MIRIPUKO

Wananchi wametakiwa kushikiriana na taasisi mbalimbali pamoja na mashirika katika kupiga vita maradhi ya mripuko hasa {kipindupindu} yanayoathiri uchumi wa nchi na kusababisha kupotea kwa maisha ya watu hasa watoto wadogo.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum ameeleza hayo wakati akifungua kikao maalum kilicho fanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Vuga na wakutanisha wadau, watendaji na wataalam kutoka taasisi mbalimbali Nchini.

Kikao hicho ni muendelezo wa kujadili mpango maahsusi wa kujikinga na kutokomeza kipindupindu Zanzibar ulio zinduliwa rasmi october mwaka jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Amesema jukumu la kupiga vita ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar si la Wizara ya Afya pekee bali linahitaji ushirikiano kati ya Serikali na wananchi kwani ugonjwa huo tayari umeshaleta athari kubwa katika Visiwa hivi na kupoteza maisha ya watu wengi hali iliyopelekea Serekali na wadau kuunga nguvu za pamoja kuhakikisha kipindupindu kinakwisha kabisa .

Naibu Katibu Mkuu Halima alifafanua kwamba changamoto ya kudharau mazingira safi na salama ndio inayopelekea kwa kiasi kikubwa jamii kuathiriwa na maradhi ya kipindupindu hasa kwa upande wa watoto wanapokua katika harakati zao za michezo.

Alizishauri Halmashauri za Wilaya kusimamia shehia zinazo wazunguka kurejesha utamaduni wa asili wa kusafisha mazingira  sambamba na kuwasiliana kwa karibu na mamlaka zinazo simamia huduma za maji kuhakikisha wanatibu maji kwa kuweka dawa kabla ya kuwafikia watumiaji.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya kukabiliana na maafa Muhidini Ali Muhidini amewaomba wananchi kuacha tabia ya kutapisha vyoo wakati wa kutiririka kwamaji ya mvua ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo kuathiri afya za wananchi.

Pamoja na mambo mengine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika kufanikisha utekelezaji wa mpango wa kutokomeza kipindupindu Zanzibar Shirika la kuhudumia Watoto ulimwengunini {UNICEF}kwa kushirikiana na shirika la misaada la Korea {KOICA} wameanzisha mradi wa“maliza kipindupindu Zanzibar” unao jumuisha Wilaya za Mjini,Magharibi “a”,Magharibi “b”,Micheweni na Wete.

Akiwasilisha mpango maalum wa kutokomeza kipindupindu Zanzibar mhandisi wa mazingira kutoka jumuiya ya uhandisi na uhifadhi wa mazingira {EEPCO} Alfred Julias Shayo ameeleza lengo kuu la mpango huo ni kusaidia utekelezaji wa mpango wa Taifa unaolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma bora ya maji,afya,na usafi wa mazingira katika kujikinga zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Alieleza kwa mujibu wa ripoti ya mapato na matumizi ya kaya (HBS) ya mwaka 2014/2015 inaonesha asilimia 17% ya wakaazi wa Zanzibar hawatumii vyoo na hujisaidia katika maeneo ya wazi hasa katika sehemu za fukwe za bahari  ikilinganishwa na asilimia 58.7% ya wanaotumia vyoo katika kaya zao.

Nao washiriki wa kikao hicho wameshauri katika azma ya kumaliza kipindupindu Zanzibar nguvu kubwa zinapaswa kuelekezwa katika kuzipatia Halmashauri vifaa vya kufanyia usafi ikwemo magari ya kubebea taka taka sambamba na kujenga uelewa kwa Wananchi juu ya namna bora ya kuweza kumaliza kipindupindu Zanzibar

 

 

 

WAZAZI NA WALEZI WALIO WENGI HAWANA TABIA YA KUZUNGUMZA NA WATOTO WAO JUU YA ELIMU YA MAZINGIRA

Viongozi wa Kamati za Skuli Madalizi na Msingi za Wilaya ya Mkoani, wamaetakiwa kuzungumuza na  Wazazi na Walezi wa Watoto ili kufahamu Afya zao  hasa katika kipindi cha Makuzi yao.

Akizungumuza  na Kamati za Skuli katika kituo cha Waalimu TC Mizingani  Wilaya ya Mkoani  Mkoa wa Kusini Pemba   Nd: Riziki   Mohamed   Juma  Afisa   Ukimwi, Afya  ya Uzazi na Madawa ya Kulevya Unguja  wakati  wa mafunzo ya   Afya ya Uzazi   kwa Watoto Wao

Amesema kuwa  lengo la kuwapatia elimu hiyo  nikuwapatia uwezo wa kudhibiti na kupambana na  matendo ya udhalilishaji katika maeneo yao ya kazi  kulingana na Wazazi na Walezi  kuto zungumza na watoto wao  kwa kisingizio cha ugumu wa maisha hali ambayo itapelekea  kwa watoto wengi kutojua  Afya zao na kuendelea kudhalilishaji.

Nae  Nd : khamisi   Haji   Hamadi   Afisa   Stadi  za maisha Pemba amesema kuwa lengo ni kuwafikiwa jamii yote  hivyo waliopewa  mafunzo hayo nivyema kuto kaa nayo waweze kutoa kwenye jamii  ili ione umhimu wa   kuongea na mtoto kuhusu mabadiliko ya mwili.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo  Wamesema  elimu hiyo itazingatiwa  kulingana na Wazazi na Walezi  weng  i hawana tabia ya kuzungumza na watoto wao kuhusu  afya ya uzazi  ambayo hupelekea   kutojua   namna  ya kujikinga na magonjwa

error: Content is protected !!