Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA YEYOTE ATAYEBAINIKA KUDHOROTESHA SHUGHULI ZA MIRADI YA MAENDELEO

Wizara ya kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Mh Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema atahakikisha anamchukulia hatua za kisheria mtumishi yeyote atayebainika kudhorotesha shughuli za miradi ya maendeleo ya wananchi.

Mh. Mmanga ameyasema hayo huko katika bonde la umwagiliaji machigini, wilaya ya Mkoani, mkoa wa kusini Pemba.

Mh. Mmanga amesema kuwa, kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakisimamia miradi yao kipindi cha mwisho cha mkataba kwa malengo ya kufanya ubabaifu huku huduma zikisuasua bila maelezo yamsingi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza tija kwa wakulima (ERPP) katika bonde la machigini afisa mkuu idara ya umwagiliaji, Mbarouk Ali ,Mgau, amesema ni kipindi cha miezi sasa tokea kukamilisha malipo kwa shirika la umeme lakini bado hawajapatiwa huduma, hali inayodhorotesha shughuli za   wakulima wa bonde hilo.

Kwa upande wao wakulima wa bonde hilo, wamesema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la umeme ambao ungaliwasaidia katika kuvutia maji ndani ya bonde lao pamoja na ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji.

TASAKHTAR GLOBAL IMEWATAKA WANANCHI KUSHIRIKA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA

Hospitali ya binafsi ya Tasakhtar Global imewataka wananchi kushirika katika zoezi la uchangiaji damu salama linalotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo kwa ajili ya kuchangia kwa wanaohitaji huduma hiyo nchini.

Zoezi la uchangiaji wa damu litakwenda sambamba kwa kutimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari afisa habari wa hospitali hiyo Bi Maryam Viktoria Mwakanjuki amesema zoezi hilo litafanyika kwa wananchi wote  ambapo damu hiyo  itapelekwa  katika  benki ya damu ili iweze kuwanufaisha wananchi wote nchini.

Cristine Sinta Manonge ni meneja masoko wa hospitali hiyo amesema  zoezi la utoaji wa damu pia litawashirikisha wafanyakazi wa hospitali hiyo ya Global na kuwataka wananchi kutambua mchango wao.

JAMII IMESHAURIWA KUFAHAMU NA KUELEWA KIUNDANI MATUMIZI SAHIHI YA KINGA DHIDI YA UKIMWI

Jamii imeshauriwa kufahamu na kuelewa kiundani matumizi sahihi ya kinga ili kuepuka maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha maradhi ya ukimwi pamoja na kupunguza maradhi ya kijamii.
Hayo yameelezwa na kamishina wa tume ya ukimwi Zanzibar ZAC Bi Hasina Hamadi Shehe wakati alipokuwa akifungua mkutano wa waandishi wa habari hukokatika ukumbi wa tume ya ukimwi Zanzibar ZAC Shangani, amesema matumizi ya kinga yanapaswa kuzingatia mila,silka na desturi ya wazanzibar kwa lengo la kuepusha upotoshaji.
Akiwasilisha mada ya mpango mkakati wa kinga mkuu wa habari utetezi na mawasiliano Nd: Sihaba Saadati amesema ifahamike kuwa utumiaji kinga unalenga zaidi makundi maalum kwa nia ya kumkinga mwenza wake na maambukizi ya maradhi mbalimbali.
Nae afisa ufuatiliaji na tathmini Nd: Gharib Said Gharib amesema ripoti walioifanya katika wilaya kumi na moja za Unguja na Pemba wamebaini kuwa jamii haijahamasika kutumia kinga ipasavyo.
Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na tume ya ukimwi Zanzibar ZAC na wamewashirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Zanzibar.

HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA MTUMISHI ATAEBAINIKA KUZOROTESHA MIRADI YA WANANCHI

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema atahakikisha anamchukulia hatua za kisheria mtumishi yeyote atayebainika kudhorotesha Shughuli za miradi ya maendeleo ya Wananchi.

Mh. Mmanga ameyasema hayo huko katika bonde la umwagiliaji Machigini, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Mh. Mmanga amesema kuwa, kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakisimamia miradi yao kipindi cha mwisho cha mkataba kwa malengo ya kufanya ubabaifu huku huduma zikisuasua bila maelezo yamsingi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza tija kwa wakulima (ERPP) katika bonde la Machigini Afisa MkuuIdara ya Umwagiliaji, Mbarouk Ali Mgau, amesema ni kipindi cha miezi sasa tokea kukamilisha malipo kwa shirika la umeme lakini bado hawajapatiwa huduma, hali inayodhorotesha shughuli za   wakulima wa bonde hilo.

Kwa upande wao wakulima wa bonde hilo, wamesema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la umeme ambao ungaliwasaidia katika kuvutia maji ndani ya bonde lao pamoja na ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji.