Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

WALIMU NA WAZAZI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANAFUNZI

Walimu na wazazi wametakiwa kushirikiana pamoja katika kusimamia masuala ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri ofsi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ Shamata Shaame Khamis katika sherehe za kuwapongeza wanafunzi waliofaulu mchepuo na vipawa wilaya ya micheweni.

Amesema mashirikiano ya pamoja ndio njia pekee ambayo itawawezesha wanafunzi kuweza   kufanya vizuri katika mitihani yao  na watakapokosa mashirikiano hawataweza kufanya vizuri.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Omari Issa Kombo amesema ili kuweza kutatua changamoto katika sekta ya elimu ni lazima kila mmoja awajibike kwa nafasi yake.

Akitoa neno la shukrani, mkurugenzi wa halmashauri hiyo Suleiman Juma Pandu, amepongeza juhudi zinazochukuliwa na walimu katika kuhakikisha ufaulu wa wanaffunzi unaongezeka micheweni.

Nao baadhi ya wanafunzi waliokabidhiwa zawadi hizo wamewataka wanafunzi kutilia mkazo katika masomo yao ili waweze kufikia malengo yao.

 

WATENDAJI WA WIZARA YA KILIMO WATAKIWA KUIMARISHA KILIMO ILI KUFIKIA LENGO LA SERIKALI

Waziri wa kilimo maliasili, mifugo na uvuvi zanzibar, Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri, amewataka watendaji wa wizara hiyo wanaoshughulika na uoteshaji na ugawaji wa miche, kusimamia na kufatilia uoteshwaji wa miche inayotolewa ili lengo la serikali la kuimarisha kilimo liweze kufikiwa.

Mh. Mmanga ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara fipi yakutembelea nasari za kuotesha  miche ya mikarafuu huko mkata maini na chanjaani wilaya ya chake chake.

Mh. Mmanga amesema, iwapo maafisa watasimamia vyema katika malezi ya miche itakayotolewa itasaidia miche mengi kustawi zaidi kwa kuisaidia serikali kuweza kutimiza malengo yake ya kunyanyua wananchi.

Afisa mdhamini wizara ya kilimo pemba, Sihaba Haji Vuai, amesisitiza kwa watendaji hao kuwaelekeza wananchi kupeleka maombi kwa masheha wao , ili hesabu halisi ya mahitaji iweze kupatikana mapema.

Kwa upande wao, wafanyakazi wa nasari za miche ya mikarafuu, Juma Kombo na Ali Muhammed, wameahidi kusimamia vyema taratibu zinazohitajika, ili kukamilisha malengo ,huku wakiiomba serikali kupitia wizara ya kilimo, kuwatatulia changamoto ya upatikanaji wa maji na ufinyu wa wafanyakazi , katika kuimarisha zao la karafuu.

WALIMU WAKUU NDIO WENYE JUKUMU LA KUSIMAMIA KAZI KWA WALIMU WENGINE ILI KULETA MAENDELEO

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali  Mhe Riziki Pembe Juma amesema walimu wakuu ndio wenye jukumu la kusimamia kazi kwa walimu wengine ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu nchini.

Akizungumza  wakati akimtambulisha naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe Simai Mohamed Said kwa walimu wakuu wa skuli za sekondari za unguja katika ukumbi wa skuli ya haille sselasie, amesema kuna baadhi ya walimu wamekuwa wanaendelea kuwatoza pesa wanafunzi kwa visingizio mbalimbali hali ambayo serikali ilipiga marufuku suala hilo.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitowafumbia macho walimu wenye tabia hiyo na kuwataka walimu wakuu kuwafuatilia walimu hao ili kutimiza azma ya serikali ya kutoa elimu bure kwa wote.

Akizungumzia sula la kambi kwa wanafunzi Mhe Riziki amewataka walimu wakuu kuhakikisha kuwa kambi zinazoshughulikia wanafunzi lazima kuwepo walimu wasimamizi na pamoja na kuhakikisha kambi zote zinakuwa na mazingira mazuri ya kuridhisha.

Amesema haitaruhusika kambi yeyote bila ya kuwepo mwalim msimamizi ambapo pia amewataka kuacha kuwachanganya wanafunzi wa kike na wa kiume pamoja ili kuepusha vishawishi vitakavyoweza kuwaharibia masomo yao.

Nae Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amewataka walimu kutovunjika moyo kutokana na ugumu wa kazi na badala yake kua na uzalendo wa kujitolea ili kuleta maendeleo katika elimu.

Akitolea ufafanuzi juu ya wanafunzi waliofeli kidatu cha pili na waliotakiwa kurejea darasa, naibu katibu mkuu taaluma Bi Madina Mjaka Mwinyi amesema ni lazima wanafunzi hao warudi skuli kuendelea na masomo yao kwa kuwapangia utaratibu maalum na sio kubaki nyumbani, kwani ni haki yao kuendelea na masomo hadi kidatu cha nne.

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA NA WANAHARAKATI WA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Serikali  na jamii imeshauriwa kuendelea kushirikiana Asasi za kiraia na wanaharakati wa utetezi wa haki za Binadamu kwa kuwa mchango wao kwa jamii ni mkubwa.

Ni kauli iliyotolewa na  mkurugenzi wa  mtandao wa watetezi wa haki za binadamu tanzania  (THRDC) ndugu onesmo olengurumo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu ya mwaka 2018 ambapo amesema  asasi za kiraia  ndizo zinazowafikia wananchi  walioko pembezoni ambako  jicho la serikali halijawafikia.

Naye wakili wa taasisi hiyo Deogratias Bwire amesema matukio mengi ya ukiukwaji wa sheria na unyanyasaji ama ule wa kijinsia yamekuwa yakiibuliwa na wadau wakiwemo wa asasi za kiraia na kusaidia serikali kufuatilia na kubaini hali halisi.

Mkutano huo umefungwa na balozi wa sweden nchini Tanzania bwana  Anders Sjoberg ambapo  alielezea namna suala la haki za binadamu linavyohusiana na maendeleo  na ustawi wa jamii.