Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

HUDUMA ZA MAKTABA KATIKA SKULI MBALIMBALI IMELETA MABADILIKO YA UFAULU

Afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali mohamed salum amesema kuwepo kwa huduma za maktaba katika skuli mbalimbali imeleta mabadiliko ya ufaulu wa wanafunzi wa msingi na sekondari katika matokeo yao ya mitihani ya taifa kutokana na   kupata muda muafaka wa kusoma vitabu.

Mdhamini mohamed amesemahayoukumbiwashirika la maktabachakechakewakatiakifunguamafunzoyakuziboreshanakuziimarishamaktabakwawakutubikutokataasisizaserikalinabinafsiambazozinatowahudumazamaktabakwawanafunzinajamii, nakusesemakuwasuala la kusomavitabunieneomuhimukwawanafunzikujifunza mambo mbalimbali.

Akielezealengo la mafunzohayomratibuwashirika la maktabatawi la pemba mwache mohamed amesemanikukumbushanamajukumuyaokwakuhakikishavituohivyovinafanyakaziinavyotakiwa.

Jumlayamadanneziliwasilishwakatikamafunzohayonajudiliwa, ambapoilibainikakuwawanafunziwamehamasikakusomavitabunavitabuvingivikoamaskulinilakinihakunamaeneoyakitaalamuyakuhifadhiavibatuhivyo.

 

 

ASASI ZA KIRAIA ZINANAFASI KUBWA KATIKA KUWASHAJIHISHA WANANCHI KATIKA KUTELEKEZA MAENDELEO

Mwakilishi  wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa –UNDP-Zanzibar  Rukiya Wadoud amesema asasi  za kiraia zinanafasi kubwa katika kuwaelimisha na kuwashajihisha wananchi kushiriki katika kutelekeza malengo ya maendeleo endelevu.

Akizungumza na viongozi wa shehia, dini na watu mashuhuri wa Wilaya ya Micheweni , Rukiya Wadoud amesema ili malengo hayo yaweze kufanikiwa ,lazima kuwepo na ushirikiano wa viongozi kutoka asasi mbali mbali.

Mapema akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mtadao wa Asasi za Kiraia Zanzibar –ANGOZA- , Asha Aboud Mzee amewataka viongozi hao  kutumia nafasi kuihamasisha jamii kushiriki kutelekeza malengo ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo Mohammed Nassor Khamis na John Shimba Shija wameahidi kuifikishia jamii elimu waliyoipata ili kuona wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza malengo hayo.

TUTAENDELEZA UTAMADUNI WA KUBADILISHANA UZOEFU KWA PANDE MBILI ZA MUUNGANO

Mkuu wa mkoa mjini magharib Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema serikali ya mkoa wa mjini magharibi itaendeleza utamaduni wa kubadilishana uzoefu kwa pande mbili za muungano katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji ili kuona lengo la serikali la kuleta maendeleo wananchi wake linafikiwa.

Akizungumza katika muendelezo wa ziara kwa mkoa wa rukwa Mhe Ayoub amesema pamoja na kutekeleza maagizo na maelekezo ya serikali, uongozi wa mkoa wa mjini mgharibi utendelea kushirikiana kwa karibu na mikoa mbalimbali katika kujifunza na kuongeza thamani ya bidhaa zinazopatikana ndani ya nchi.

Aidha Mh: Ayoub ameridhishwa na uwezo wa chinjio la saafi katika maeneo ya uchinjaji na uzalishaji bidhaa zipatikanazo kiwandani hapo na kuahidi kushauri vizuri serikali katika uimarishaji wa machinjio mbalimbali nchini.

Akitoa maelezo ya chinjio hilo afisa mfawidhi wa kituo cha uchunguzi wa maradhi ya wanyama na daktari mkuu wa kiwanda cha nyama cha  saafi Dr Kaini Martin Kamwela amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe miatatu kwa siku pamoja na ziada ya wanyama wadogo wadogo kama mbuzi na kondoo.

Akizunguza mara baada ya kupokea ujumbe huo mkuu wa wilaya ya sumbawanga Dr Khalfany Haule ameuomba uongozi wa serikali ya mkoa wa mjini kutumia uwezo na nafasi walionayo kuwatafutia wawekezaji kiwanda cha saafi katika mifugo na maziwa kutokana wingi wa ng’ombe walipo wilayani hapo.

VIJANA WATAKIWA KUONDOSHA DHANA YA KUONA KUWA KAZI YA KILIMO NI YA WATU WA VIJIJINI

Waziri wa biashara na viwanda, balozi Amina Salum Ali, amewataka vijana kuondosha dhana ya kuona  kuwa kazi ya kilimo ni ya watu wa vijijini.

Balozi Amina amesema kilimo hasa kinachozingatia maelekezo  ya  kitaalamu kimekuwa ni mkombozi mkubwa wa  maisha ya watu walioamua kujikita katika sekta hiyo ikiwemo kilimo cha mboga mboga ambacho kimekuwa na tija, hivyo amewataka vijana  kuelekeza nguvu zao ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

Akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya kilimo hai kwa maendeleo endelevu, kwa vijana 18  balozi Amina amesema serikali imekuwa katika jitihada za kuhakikisha vijana wanajiimarisha katika ujasiriamali na kuwajengea mazingira bora ya kuwapatia fedha za mkopo waweze kuendesha vyema shughuli zao za kujitegemea.

Wafadhili wa mafunzo hayo taasisi ya kuongeza kasi ya maendeleo Zanzibar milele Zanzibar foundation, katika taarifa iliyomwa na afisa maendeleo, biashara na uchumi jamii, Nd. Ghalib Khamis Machano, amesema wanawakaribisha wafadhili kuwasaidia vijana waliopata mafunzo ili kuitumia vizuri taaluma waliyoipata ya kilimo hai.

Mratibu wa fursa kijani iliyoendesha mafunzo hayo, bi Agnes  Bweye, ameelezea umuhimu wa taaluma hiyo ya kilimo hai, ambapo risala ya wahitimu iliyosomwa na Kassim Maulid imependekeza maombi ya kuwezesha vijana hao kuweza kujiimarisha katika ujasiriamali.

 

 

error: Content is protected !!