Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

MATOKEO MABAYA YA WANAFUNZI YAMECHANGIWA NA WALIMU WALIOSHINDWA KUWAJIBIKA

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma skuli ya msingi na sekondari ng’ambwa, wamesema matokeo mabaya ya wanafunzi kwa mwaka 2018, yamechangiwa na walimu ambao wameshindwa kuwajibika pamoja na kuwatolea maneno ya jeuri wazazi wanapofuatilia maendeleo ya watoto wao.

Matokeo mabaya ya mitihani ya taifa katika skuli hiyo yamewafanya wazazi kukutana kujadili mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya ufaulu ambapo mzee haji hamad kombo na robart miguwa pamoja na katibu tawala wilaya ya chake chake omar khamis juma wamesema ujeuri wa walimu pamoja na kukosa uzalendo ndio sababu ya matokeo hayo.

afisa elimu na mafunzo ya amali wilaya ya chake chake , abadalla omar muya amewataka walimu kuandika barua kujieleza na kuzifikisha ofisini kwake si zaidi ya siku ya jumatano, huku mwalimu asma ali hafidh akielezea kutoridhishwa na matumizi ya simu kwa wanafunzi.

Mkuu wa wilaya ya chake chake rashid hadid rashid akizungumza kwenye mkutano huo amewataka wazazi kumpa ushirikiano ili kufanikisha kudhibiti utoro wa wanafunzi.

Mkutano ni moja ya mkikati ya serikali ya wilaya ya chake chake kuhakikisha inadhibiti utoro wa wanafunzi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi

WIZARA ZA SERIKALI ZITAKAZOHAMIA MAJENGO MAPYA KUTENGA BAJET

Naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango idd haji makame amezitaka wizara za serikali zitakazohamia katika majengo mapya yaliopo gombani kutenga bajeti maalum kwaajili ya kuhudumia majengo hayo ili yaweze kuendelea kuwa katika haiba yake.

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango zanzibar nd,Idd Haji Makame wa katika wa makabidhiano ya majengo hayo kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya quality bulding contractors huko gombani ambayo yamekamilika ujenzi wake.

Amesema wizara hizo zinawajibu wakuyalinda majengo hayo ambayo yametumia gharama za serikali, hivyo ni vyema kuyatengea bajeti maalum kwa ajili ya utunzaji ikiwemo usafi na huduma nyengine.

Akizungumza mara ya makabidhiano hayo naibu katibu mkuu wizara ya kazi,uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto bi maua makame rajab amesema jukumu liliobakia ni kwa watendaji kuweza kuyatunza majengo hayo pamoja na kukaa katika hali nzuri ili yaweze kudumu

Kwa upande wake mshauri mwelekezi katika ujenzi huo kutoka kampuni ya zancon limited nd,Mbarouk Juma Mbarouk amesema mashirikiano waliyoyapata yamelekea kukamilika ujenzi huo katika wakati uliyopangwa huku mkurugenzi mtendaji wakampuni ya quality bulding contractors Ahamis Ali Said ambayo iliyojenga majengo hayo ameiomba serikali kuendelea kuwa tumilia wakandarasi wa zawa.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo afisa mdhamini wizara ya fedha na mipango nd,Ibrahim Saleh Juma amesema ujenzi huo ulioanza septemba mwaka 2016 na kukamika tarehe 31 machi mwaka huu utaondosha shida ya ufinyu wanafasi iliyokuwa ikiwakabili.

 

SERA YA VIWANDA INATEKELEZWA KWA MAENDELEO YA WANANCHI NA TAIFA KWA JUMLA

Serikali ya mapinduzi Zanzibar, itaendelea kulinda viwanda vyake ili kuhakikisha sera ya viwanda inatekelezwa kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla.

Amesema mataifa yaliyoendelea yamefikia hatua hiyo kutokanan na kuwa na viwanda na kwamba Zanzibar itaimarisha viwanda mbali mbali vikiwemo vya kusindika matunda zikiwemo tungule.

Waziri wa wizara ya biashara na viwanda, Balozi Amina Salum Ali, ameyaema hayo wakati akizungumza na ushirika wa mtule amcos limited katika kijiji cha Paje ulionzisha kiwanda cha kutengeneza tomato paket .

Amesema serikali  itaendelea  kuhakikisha inasaidia nguvu wananchi wake wakiwemo wakulima ili kuona  wanapata kipato kupitia viwanda vya ndani.

Akisoma risala ya wanaushirika wa mtule amcos limited katibu wa ushirika huo, Ali Fadhil Ali, amesema ushirika wao unakabiliwa na matatizo mbali mbali  ikiwemo umalizaji wa kiwanda na upatikanaji wa vibali kutoka mamlaka husika ikiwemo ZBS na TBS.

Ushirika huo una wanachama 139 wakiwemo wanawake 52 na wanaumme 87 ambapo kila mmoja anamiliki shamba lake la zao la tungule.

WALIMU NA WAZAZI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANAFUNZI

Walimu na wazazi wametakiwa kushirikiana pamoja katika kusimamia masuala ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri ofsi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ Shamata Shaame Khamis katika sherehe za kuwapongeza wanafunzi waliofaulu mchepuo na vipawa wilaya ya micheweni.

Amesema mashirikiano ya pamoja ndio njia pekee ambayo itawawezesha wanafunzi kuweza   kufanya vizuri katika mitihani yao  na watakapokosa mashirikiano hawataweza kufanya vizuri.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Omari Issa Kombo amesema ili kuweza kutatua changamoto katika sekta ya elimu ni lazima kila mmoja awajibike kwa nafasi yake.

Akitoa neno la shukrani, mkurugenzi wa halmashauri hiyo Suleiman Juma Pandu, amepongeza juhudi zinazochukuliwa na walimu katika kuhakikisha ufaulu wa wanaffunzi unaongezeka micheweni.

Nao baadhi ya wanafunzi waliokabidhiwa zawadi hizo wamewataka wanafunzi kutilia mkazo katika masomo yao ili waweze kufikia malengo yao.

 

error: Content is protected !!