Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

JUHUDI ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KATIKA KUONA MATATIZO YANAYOYAKABILI BARA LA AFRIKA

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema juhudi za pamoja zinahitajika katika kuona matatizo yanayoyakabili bara la afrika yanatatuliwa kwa kutumia nguvu za pamoja za wananchi wa bara hilo.

Amesema mataifa ya afrika ni lazima yaendelee kushirikiana kutokana na historia yao ya kiutamaduni, kisiasa, mila na kiuchumi

WANAWAKE DUNIANI WAMETAKIWA KUJITAMBUA, KUJITATHAMINI

Siku chache baada ya madhimisho ya siku ya wanawake duniani, wanawake nchini wametakiwa  kujitambua, kujitathamini pamoja na kuacha kuvaa nguo zisizo na maadili.

Kauli hiyo imetolewa na afisa mratibu wa shughuli za serikali ya mapinduzi ya zanzibar upande wa tanzania bara bi mwanaisha ramadhan kondo wakati wa mahojiano maalumu na zbc.

Bi mwanaisha amesema wapo baadhi ya wanawake ambao wanatarajiwa kuwa akinamama wa baadae wanavaa nguo zinazonyesha sehemu za maungo yao.

Hafsa omar khamis  ni afisa mipango wa ofisi ya uratibu wa shughuli za serikali ya mapinduzi zannzibar apande wa tanzania bara amewataka wanawake kutumia siku hiyo vizuri na kutambua kuwa wao ni kiungo katika familia na wana mchango mkubwa katika jamii.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo machi nane ya kila mwaka ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii.

DAWA ZA MALARIA ZINAZOPIGWA KATIKA NYUMBA HAZINA MADHARA

Serikali wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba imewatoa hofu wananchi kwamba dawa za malaria zinazopigwa katika nyumba zao hazina madhara  bali zinaangamiza mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya micheweni bi salama mbarouk khatib wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya tumbe ambao wamegoma kupigiwa dawa majumbani mwao

Amesema  lengo la serikali ni kuutokomeza ugonjwa wa malaria  na atasimamia ili kuhakikisha  zoezi hilo linafanikiwa na nyumba zote zinapigwa dawa.

Afisa kutoka kitengo cha malaria wizara ya afya pemba bakar omar khatib amesema wanachokifanya wanapofika kwenye nyumba ni kuwataka wakaazi wake kukunja vitu ambavyo vinaweza kuharibika na kuleta athari.

Mratibu wa mradi wa upigaji dawa faki haji faki  ametaka kuomngeza uhamasishaji ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Zoezi la upigaji wa dawa linafanyika katika shehia ambazo zimegunduliwa kesi za watu kuwa na virusi vya ugonjwa wa malaria.

 

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR PBZ KUIMARISHA HUDUMA ZA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI

Benki ya watu wa zanzibar pbz   imeimarisha

huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwenye matawi yake yote yaliopo  zanzibar lengo ni kuwarahisishia wananchi huduma hizo baada ya kupata kibali kutoka benk kuu ya tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji p.b.z juma ameir hafidh hapo ofisini kwake mpirani.

Amesema  huduma hiyo itamrahisishia mwananchi na mfanya biashara kuweza kununua au kuuza fedha za kigeni ambazo zinakubalika kimataifa kwa wakati kupitia benki ya watu wa zanzibar.

Nd juma amesema benk ya pbz pia inatarajia baada ya miezi ijayo kuongeza huduma zake nchini .

 

error: Content is protected !!