Category Archives: Kimataifa

habari za nje ya nchi

RAIS WA ALGERIA ABDELAZIZ BOUTEFLIKA ATAWANIA URAIS KWA MUHULA WA TANO

Rais wa algeria Abdelaziz Bouteflika atawania urais kwa muhula wa tano wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika nchini humo mwezi aprili. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 na ambaye amekuwa rais tangu mwaka 1999, atawania wadhifa wake kwa mara nyingine. Watu wake wa karibu wanasema hali yake ya kiafya sio kigezo cha raia huyo kutowania urais, kwa sababu chama chake kimeonesha imani ya kutaka aendelee kuongoza. Tangu mwaka 2013, Rais bouteflika, amekuwa akitumia gari la magudumu baada ya kupata kiharusi, hata hivyo kiongozi huyo anakumbukwa kwa kusadia nchi yake kumaliza vita vya wenyewe kwa wenywe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 kabla ya kuingia madarakani.

 

 

ZAIDI YA WATU 500 WAFA KWA EBOLA DRC

Wizara ya afya nchini jamhuri ya kidemokrasi ya kongo imesema imefika zaidi ya watu 500 waliofariki kutokana na virusi vya ebola. Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana imeeleza kuwa tokea kuibuka kwa ugonjwa huo mashariki mwa kongo, watu 505 wamekufa, na watu 271 wametibiwa. Ugonjwa huo ulizuka mwezi juni mwaka jana muda mfupi baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza kumalizika kwake katika eneo la magharibi mwa kongo. Kwa mujibu wa waziri wa afya wa nchi hiyo, oly kalenga, amesema tangu mwezi agosti, zaidi ya watu 70 elfu wamepatiwa chanjo ya ebola. Maafisa wa afya na mashirika ya kutoa misaada wamekuwa wakikabiliwa na matatizo katika kupambana na ugonjwa huo ikiwemo makundi mbali mbali ya wapiganaji yanaendesha operesheni zake, yakiwa yanagombania rasilimali za taifa hilo.

MAREKANI NA CHINA KUJIPA MATUMAINI YA KUWEZA KUTULIZA MVUTANO WAO

Marekani na China Wanaonyesha Kujipa Matumaini ya Kuweza Kutuliza Mvutano wao wa Kibiashara. Rais wa Marekani Donald Trump amesema baada ya Mazungumzo pamoja na Makamo wa Rais wa China Liu He,"makubaliano muhimu ya kibiashara yatafikiwa."Mjumbe wake katika mazungumzo ya biashara pamoja na China, Robert Lightizer amesema pia "maendeleo yameweza kupatikana" wakati wa mazungumzo yao. Rais Xi Jinping wa China ameandika katika risala yake anataraji pande hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika hali ya kuheshimiana. Pindi makubaliano yakishindwa kufikiwa hadi Machi mosi inayokuja, rais Trump anapanga kuzitoza ushuru wa asilimia kati ya 10 na 25 bidhaa zote zitakazoingia Marekani kutoka China.

MDC YAPINGA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

Chama kikuu cha upinzani nchini zimbabwe mdc kimelaani vikali ukandamizwaji ulioshuhudiwa wakati wa kuzimwa kwa maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo. Kwa mujibu wa mashirika ya mawakili kwa ajili ya haki za binadamu yamebainisha kuwa zaidi ya watu 800 wamekamatwa wakiwemo wafuasi wa upinzani na wale wa mashirika ya kiraia. Katika mkutano na waandishi wa habari, chama kikuu cha upinzani cha movement for democratic change (mdc), kimelaani ukandamizaji wa siku za hivi karibuni nchini humo.  Hata hivyo serikali ya zimbabwe, inaushtumu upinzani kuandaa maandamano hayo na kuchochea vurugu.