Category Archives: Kimataifa

habari za nje ya nchi

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI VENEZUELA JUAN GUAIDO AMEITISHA MAANDAMANO

Kiongozi wa upinzani nchini venezuela juan guaido ameitisha maandamano ya nchi nzima ili kuongeza shinikizo dhidi ya rais nicolas maduro, wakati taifa hilo likiingia siku ya tatu bila ya umeme. Kukatika kwa umeme kumeongeza mvutano wa kisiasa baina ya guaido anayetambulika kuwa kiongozi halali na nchi zaidi ya 50 na maduro ambaye anang'ang'ania madaraka. Guaido mwenye umri wa miaka 35, na mkuu wa bunge la venezuela, awali aliwaambia maelfu ya wafuasi kwamba hivi karibuni ataanza ziara ya nchi nzima kabla ya kuendesha maandamano makubwa katika mji mkuu caracas. Maduro pia aliwataka wafuasi wake kuupinga ubeberu katika maandamano ambayo yanaashiria miaka minne tangu marekani ilipoitangaza venezuela kuwa "kitisho" kwa usalama wake na kuiwekea vikwazo.

NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES IMEANGUKA NA KUUA ABIRIA WOTE

Taarifa ya kampuni ya ndege ya ethiopian airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri katika ndege iliyopata ajali wote wamekufa. Msemaji wa kampuni hiyo asrat begashaw amesema ndege ya kampuni ya ethiopia aina ya boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka adis ababa kuelekea nairobi imeanguka leo asubuhi. Taarifa ya shirika la ndege la ethiopian airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege hiyo dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa adi ababa na wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamekufa. Kampuni hiyo inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo

PANDE HASIMU NCHINI YEMEN ZIMEKUBALIANA KUONDOA VIKOSI HODEIDA

Serikali ya yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondowa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa hodeida na katika bandari za salif na ras isa. Umoja wa mataifa umesema hayo ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa. Bandari ya hodeida ni muhimu kwani ndiko inakofikia misaada ya jumuia ya kimataifa kwa ajili ya wananchi kutokana na nchi hiyo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuhamishwa wanajeshi wa pande zinazohasimiana kutoka mji wa hodeida ni kiini cha makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa desemba iliyopita nchini sweden.

RAIS WA ALGERIA ABDELAZIZ BOUTEFLIKA ATAWANIA URAIS KWA MUHULA WA TANO

Rais wa algeria Abdelaziz Bouteflika atawania urais kwa muhula wa tano wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika nchini humo mwezi aprili. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 na ambaye amekuwa rais tangu mwaka 1999, atawania wadhifa wake kwa mara nyingine. Watu wake wa karibu wanasema hali yake ya kiafya sio kigezo cha raia huyo kutowania urais, kwa sababu chama chake kimeonesha imani ya kutaka aendelee kuongoza. Tangu mwaka 2013, Rais bouteflika, amekuwa akitumia gari la magudumu baada ya kupata kiharusi, hata hivyo kiongozi huyo anakumbukwa kwa kusadia nchi yake kumaliza vita vya wenyewe kwa wenywe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 kabla ya kuingia madarakani.

 

 

error: Content is protected !!