Category Archives: Kimataifa

habari za nje ya nchi

MWELEKEO WA HALI YA UCHUMI WA ZANZIBAR KWENDA SAMBAMBA NA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MAENDELEO

Makamu  wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif  Ali iddi amesema mwelekeo wa haliya Uchumi  wa Zanzibar  kwa mwaka 2020 unategemea kwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo, MKUZA  na ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Amesema   Pato la Taifa lilitarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 7-8 kwa mwaka 2020 kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa shughuli mbali mbali za Kiuchumi na Mendeleo.

Balozi  Seif Idd alisema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mwaka wa Fedha wa 2020/2021 kwenye Mkutano wa kumi na tisa wa Baraza la Tisa la wawakilishi ulioanza  Rasmi leo ili  kujadili Bajeti ya  Serikali ya Mapinduziya Zanzibar.

Hata hivyo Balozi Seif alifafanua kwamba kutokana na janga la Virusi vya CORONA {covid – 2019}, Uchumi wa Taifa unatarajiwa kukuwa kwa kasi ya Chini ya asilimia hii itatokana na kuyumba kwa sekta za Uchumi ikiwemo Utalii, Biashara, uwekezaji na kupungua kwa mapato ya Serikali.

Makamu  wa  Pili  wa  Rais  wa  Zanzibar  aliliomba  Baraza la  Wawakilishi  liidhinishe jumla yashilingi bilioni sabini natano,  kumi na tano milioni, laki tano na thalathini natatu elfu { 75,015,533,000 } kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais nataasisi zake kwa ajili ya kutekeleza programu 11ndani ya kipindi cha fedha cha Mwaka 2020/2021.

Wakichangia  bajeti hiyo wajumbe wa  baraza la wawakilishi  wameishauri ofisiHiyo  kujipanga vyema zaidi na kumarisha  huduma  katika sekta zake mtambukaIkiwemo kupambana na dawa za kulenya, huduma kwa watu wenye ulemavu Mazingira.

 

 

KIPINDI CHA MWEZI WA RAMADHANI KUMEKUWA NA BIDHAA ZA VYAKULA ZA KUTOSHA KATIKA MASOKO.YA ZANZIBAR

Wafanyabiashara na baadhi ya Wananchi wamesema katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumekuwa na bidhaa za vyakula za kutosha katika Masoko.ya Zanzibar

Wamesema Mazao kama Ndizi, Mihogo, Majimbi na Madukani katika Ramadhani hizi za mwazo vimekuwa vingi na bado bei zake ni nafuu.

Wamesema tatizo liliopo ni upatikanaji wa Fedha kwa watu jambo ambalo litawapa shida katika upatikanaji wa bidhaa hizo kwaajili ya Futari.

MH. MGENI HASSAN AMESEMA WANAWAKE WANA NGUVU KUBWA KATIKA NGAZI ZOTE ZA KIUCHUMI, KISIASA ,KIJAMII

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma amesema Wanawake Wana nguvu kubwa katika ngazi zote za Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii ya kulifanya Taifa kupiga hatua za Maendeleo

Akizungumza katika kongamano la Shamra shamra za kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Mhe Mgeni amesema katika kufikia hatua hizo Wanawake nao wako mstari wa mbele kupiga vita Umasikini ili kuwepo na usawa.

Amewataka kinamama kubadilika kwa kujiendeleza katika nyanja mbali mbali za Maendeleo ikiwemo ushiriki  kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakichangia mada zilizowasilishwa katika mdahalo huo washiriki wamevitaka vyama vya siasa kuweka miongozo ya nafasi za uongozi kwa Wanawake  katika vyama vyao ili waweze kufanikisha mawazo yao kuweza kuleta mabadiliko.

Mdahalo huo uliotayarishwa na Asasi za Kiraia zinazopigania Maendeleo ya Wanawake  Nchini, chini ya ufadhili wa UN WOMEN, umewashirikisha Viongozi   wa vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi, Viongozi wa Dini na Wanawake ukiwa na kauli mbiu ya “Ushiriki wa Wanawake ni chachu ya Maendeleo.

 

 

BALOZI ALIYETEULIWA NA GUAIDO ACHUKUA UDHIBITI WA UBALOZI NCHINI MAREKANI

Balozi aliyechaguliwa na kiongozi wa upinzani wa venezuela juan guaido kuwa mwakilishi wa nchi yake nchini marekani carlos vecchio, ametangaza kuchukua udhibiti wa maeneo matatu nchini marekani ambayo kidiplomasia ni mali ya venezuela. Vecchio ameingia katika majengo mawili ya jeshi la venezuela mjini washington, huku waziri anayehusika na masuala ya ushauri gustavo marcano aliyeteuliwa na guaido akiuchukua ubalozi mdogo mjini new york. Waziri wa mambo ya nje wa venezuela jorge arreaza ambaye ni mtiifu kwa rais nicolas maduro amelaani hatua hiyo, akiita kuwa ukaliaji haramu na wa kimabavu. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya marekani amethibitisha kwamba serikali ya rais donald trump imeridhia hatua hizo zilizochukuliwa na upande wa guaido, ambaye imemtambua rasmi kama kiongozi wa mpito wa venezuela.

error: Content is protected !!