Category Archives: Mpira wa Miguu

MAJINA NANE YA WAJUMBE WA KAMATI YA UHAMASISHAJI WAKATI WA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI CUP

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Omar Hassan Kingi ametangaza Majina Nane ya Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji wakati wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup.

Kamati hiyo itakayojumuisha Wajumbe kutoka Zanzibar na Tanzania Bara itaongozwa na Mwenyekiti Taufiq Salim Tturkey ambae ni mbunge wa Jimbo la Mpendae na Wajumbe wengine saba ambao ni Hassan Mussa Ibrahim (Has T), Salum Issa Ameir, Mwanahawa Rajab Iddi, Khamis Mwinjuma (Mwana Fa) Jeri Muro,  Salama Jabir na Ali Saleh (Albato).

Akitangaza Majina hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Tabia Maulid Mwita amesema lengo la Kamati hiyo ni kunogesha  na kuwahamasisha Wananchi kupitia Wasanii wa Sanaa za Asili, Maigizo na kizazi  kipya ili kuwezesha kufana kwa Sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha amesema Kamati hiyo itakuwa na Majukumu ya kuratibu na kusimamia Wasanii pamoja na upatikanaji wa Fedha kutoka kwa Wadau wa michezo, Wafadhili na Taasisi Binafsi kwa ajili ya uendeshaji wa Michuano hiyo.

Kingi pia ameitumia fursa hiyo kuwashajihisha Wananchi kushiriki kwa wingi katika Michuano hiyo yenye mnasaba wa kuyaenzi   Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Hamasa za Wasanii mbali mbali zitatumbuizwa kabla ya  Mechi, wakati wa mapumziko na baada ya Mechi.

 

MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA MICHEZO _WATOTO MAPINDUZI CUP

Hafla ya kukabithiana vifaa vya michezo  vitakavyotumika  katika michezo  ya ZBC Watoto kwa upande wa Wizara ya Habari  imejihakikishia kujipanga na Michezo na kuhakikisha inapewa kipaombele  hasa kwa vijana.

Vifaa hivyo vya Michezo vimetolewa na Mfanyabiashara Nd. Mohammed Raza amesema msaada huo unatokana na juhudi za Serikali katika Kuinua Michezo.

Vifaa mbalimbali vimetolewa kwa ajili ya Michuano hiyo vikiwemo Jezi, Vikombe pamoja na Mipira.

YAMLE YAMLE CUP

Mashabiki wa Meli Nne City na Mbirimbirini wameendelea na tambo na majigambo kuelekea nusu Fainali ya michuano ya Yamle Yamle Cup inayotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Mao Zedong’s siku ya Jumamosi na Jumapili.

Wiki hii.

Wakizungumza na ZBC michezo shabiki wa Timu zote mbili wamejigamba kuhakikisha wanashinda na kuweza kuingia Fainali na kulichukuwa Kombe hilo.

Aidha Wazee na Mashabiki wameiomba kamati ya  Michuano hiyo kuendelea kufanyika kwa Michuano hiyo katika kiwanja cha Magirisi Arena kwa hatua za Awali ili Wakaazi wa maeneo hayo wanufaike.

Nusu Fainali ya kwanza ya Michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa  Mao Zedong's.

YAMLE YAMLE CUP

Kamati ya Mashindano ya Yamle Yamle Cup imetangaza ratiba ya Nusu Fainali ya Mashindano hayo ambazo zinatarajiwa kuchezwa Novemba 14 na 15 katika Uwanja wa Mao ze dong.

Kamati hiyo imekutana  katika Ukumbi wa ZBC Radio Rahaleo ambapo Mratibu wa mashindano hayo  Sadiki Ali amesema nusu Fainali ya kwanza itawakutanisha Timu ya Meli Nne City ambao zamani wanajulikana kwa jina la New Juve dhidi ya Mbirimbini Mchezo ambao utasukumwa  Jumamosi ya Novemba  14 na siku ya Jumapili Novemba 15 Timu ya Mboriborini watavaana na Ndugu zao Timu ya Munduli Heroes ambao zamani walikuwa wakiitwa Juve Camp.