Category Archives: Biashara

habari za biashara

WAKULIMA WA MWANI WA KIJIJI CHA PAJE WAPATA KHOFU JUU YA KILIMO CHAO

Wakulima wa mwani wa kijiji cha paje wameuomba uongozi wa wizara ya kilimo kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuangalia harakati za watalii za michezo ya baharini katika fukwe za paje kwani zimeanza kuwajengea hofu juu ya kilimo chao cha mwani.

Wakulima hao wameiambia ZBC kuwa watalii wanafanya   michezo ya maputo smoklin karibu na maeneo ya fukwe wakati ambapo kilimo cha mwani kikiwa kinaendelea.

Wamesema kuwa ingawa utalii una faida sana katika taifa  lakini ni vyema taasisi husika zikakaa pamoja kuwapangia maeneo maalum ambayo wao watafanya michezo yao hiyo  na harakati za kilimo cha mwani zikiendelea.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema watakaa pamoja na mamlaka ya uwekezaji ili kutafuta muafaka wa tatizo hilo bila ya kutokea athari yoyote.

VYUO VYA MAFUNZO ZANZIBAR VYAEKA UTARATIBU MAALUMU WA KUENDELEZA KILIMO

Uongozi wa vyuo vya mafunzo zanzibar , umesema uweka utaratibu maalumu wa kuendeleza kilimo, ili kuwafanya wanafunzi wa vyuo vya mafunzo kuwa wazalishaji wanapomaliza muda wa kutumikia vyuo hivyo.

Hayo yamesema na Kamishna wa vyuo vya Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla wakaati wa zoezi la uzinduzi wa uvunaji wa mpunga katika kambi ya chuo cha Mafunzo Tungamaa Wilaya ya Wete.

Aidha Kamishna Ali Abdalla amesema zoezi hilo la uvunaji wa Mpunga katika mabonde ya Tungamaa , umelenga kuongeza uzalishaji wa chakula kwa wanafunzi wa vyuo vya mafunzo.

Naye Mkuu wa kambi la chuo cha Mafunzo Tungamaa, Mkaguzi Hafidh Haji Mcha, amemshukuru kamishna kwa uwamuzi wake wa kushiriki zoezi la uvunaji wa Mpunga katika bonde la Tungamaa.

Mkaguzi Hafidh , amesema zoezi hilo la uvunaji wa Mpunga ni kuunga mkono mapinduzi ya Zanzibar ya januari , 1964.

Wananchi wamezoea kuona viongozi wanazindua majengo,barabara na huduma nyengine , lakini uwamuzi wa kamishna anaunga mkono.

Kamanda Haji amewataka wananchi kushirikiana na askari wa vyuo vya mafunzo katika kuimarisha sekta ya kilimo kwa wanafunzi.

Imekuwa ni kawaida wa askari wa vyuo vya mafunzo kuwashirikisha viongozi kwa ajili ya kuvuna mpunga ambapo msimu uliopita zoezi hilo lilizinduliwa na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman.

UJIO WA MELI MPYA YA SEA STAR 1 KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR

Ujio wa meli ya sea star 1 katika bandari ya zanzibar itapelekea kupunguza changamoto zilizokuwepo kwa wananchi wanaosafiri kutoka zanzibar, tanzania bara na tanga kwa kuweza kuwarahisishia.

Kepteni wa meli hiyo, Nasour Abubakari, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na zbc  baada ya ukaguzi wa meli hiyo ilipowasili zanzibar huko katika gati ya malindi mjini unguja.

Aidha amesema madhumini hasa ni kuweza kuunganisha kiusafiri kwa wananchi pamoja na kuwapunguzia harama na kuwapa urahisi kwa kila mwananchi.

Nae mfanyabiashara ambae ni mmiliki wa meli hiyo, salim turki, amesema nia na ndoto ya kuletwa meli hiyo ambapo itaweza kuwasaidia wananchi. Hivyo ameahidi kufanya kazi kama walivyomueleza ili kuona wananchi kuona jihudi na serikali kutatua tatizo kwa wananchi linafikiwa pamoja na wananchi kukitumia chombo hicho kitakapoanza kufanya kazi.

Naodha  mariya pamoja na msaidizi wake ambaye aliyekifikisha chombo hicho hapa nchini kutokea ugiriki amesema chombo hicho ni kimpya na kimetengenezwa nchini ugiriki mwaka 2018,ambapo kimechukua takribani siku 19 hadi kufika zanzibar.

Amesema chombo kimekuwa na ubora wa hali ya juu ambapo chombo hicho kimekuwa na ubora zaidi na kinaweza kuchukua abiria zaidi ya wananchi 1000, gari 200.

KUDHIBITI FEDHA ZA KUENDESHEA BIASHARA NI MIONGONI MWA MATATIZO YANAYOWAKABILI WAJASIRIAMALI

 

Kuweka kumbukumbu na kudhibiti fedha za kuendeshea biashara ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wajasiriamali  wengi ambayo husababisha kuzorota na hatimaye kufa biashara zao.

hayo yameelezwa skuli ya maendeleo ngwachani na muwezeshaji wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa mabaraza ya vijana ya wilaya ya mkoani Amini Omar Ali, ambayo ni utekelezaji wa mradi wa kuimarisha utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana na sharia ya mabaraza.

amesema wajasiriamali wengi wanaendesha biashara zao bila ya kuwa na mpango sahihi wa kuweka kumbukumbu ya miamala ya biashara zao hali ambayo hawapati picha halisi ya kuwa wamepata faida ama hasara.

kwa upande wa vijana hao wamesema kwa sasa wataendesha shughuli zao za kibiashara kitaalamu  na sio kimazoweya.

akiahirisha mafunzo hayo mwenyekiti wa jukavipe ali abdalla said kuyarithisha mafunzo hayo katika mabaraza yao ili yawe endelevu.

mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na jukavipe kupitia the foundation for civil society.