Category Archives: Biashara

habari za biashara

WAWILI WAKAMATWA NA MAGENDO YA KARAFUU

Watu wawili wakaazi wa konde wilaya ya Micheweni wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kaskazini pemba, baada ya kukamatwa   na magunia 18 ya karafuu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18, yaliyokuwa katika harakati za kusafirshwa nje ya nchi kinyume na sheria.

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba kamishna msaidizi mwandamizi , Mohammed Skhekhan  Mohammed , amesema tayari jeshi hilo limefungua jalada, na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mhe Omar Khamis Othman amesema kwamba  kutokana na wingi wa karafuu, zinaonyesha kwamba ni za msimu wa  mwaka jana, kwani kwa mwaka huu, bado uchumaji wa karafuu hajafikiwa kiwango hicho.

Naye mdhamini wa shirika la biashara la taifa zanzibar ofisi ya pemba Abdalla Ali Ussi , amesema kwa mujibu wa sheria ya maendeleo ya karafuu, hairuhusu mwananchi kuhifadhi karafuu nyumbani kwake na kuomba sheria zichukue mkondo wake.

MPANGO MAALUM WA KUWEKA MIUNDOMBINU BORA YA USALAMA KWENYE VITUO VYA MAFUTA

Wamiliki wa vituo vya mafuta kisiwani pemba wametakiwa kuwa na mpango maalum wa kuweka miundombinu  bora ya usalama kwenye vituo hivyo ikiwemo kuwapa mafunzo wafanyakazi wao na kuweka vifaa vya huduma ya kwanza ili waweze kujiokoa panapotokezea matatizo.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na mkuu wa operation ya kukabiliana na maafa zanzibar Shaaban Hassan Ramadhan katika ziara ya ukaguzi wa bohari na vituo vya mafuta kisiwani humo

Amesema katika ukaguzi huo wamegundua mapungufu mengi ya kiusalama huku akitoa agizo la miezi mitatu kwa wamiliki kuyafanyia kazi mapungu hayo kabla ya kutokea maafa yasiyotarajiwa

Katika ziara hiyo mkuu wa operation ya uokozi kutoka kikosi cha zimamoto ali abdi hashim amesema baadhi ya vituo havina dawa mitungi ya kisasa ya kuzimia moto wala matangi ya maji hivyo kuwa vigumu kwao kuweza kujisaidia kunapotokea tatizo

Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo vya mafuta wamesema watayafanyia kazi mapungufu madogo madogo yaliopo na yale makubwa watawasiliana na wamiliki wao kwa ajili ya kuyachukulia hatua

SMZ ITAENDELEA KUTEKELEZA AZMA YA KUWAWEZESHA VIJANA

WAZIRI wa Kazi , Uwezeshji, Wazee, Wanawake na Watoto, Modiline Kastiko  amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar (smz) itaendelea kutekeleza azma  ya kuwawezesha vijana  ili kuweza kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

kauli hiyo ameitoa wakati akimwakilisha Makamu wa Pili wa Rais katika Uzinduzi wa Ushirika wa Ufugaji kuku kwa vijana wa Mkoa wa Mjini Magharib,

Mhe, Waziri Alisema miongoni mwa azma hizo ni kuhakikisha inatatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia wizara hiyo.

Ameongeza kuwa serikali imeona umuhimu wa kuanzisha wizara hiyo ili kuona vijana wanasaidiwa katika kuwatafutia mbinu mbalimbali za kuweza kijiajiri kwa lengo la kuondokana na vitendo viovu ambavyo vitawaharibia malengo yao ya maisha.

Waziri Castico amewataka vijana kuzitumia fursa hiyo ya mradi wa ufugaji kuku kwa lengo la  kujikwamua kiuchumi na  kuwawezesha vijana wengine kupata kuku hao na kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Castico amewataka vijana hao ambao wamepata mafunzo ya ufugaji wa kuku aina ya Saso kushirikiana na vijana wenzao kwa kuwapa elimu hiyo ili na wao waweze kufaidika na mardi huo na kuondokana na umasikini.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Rashid Mohamed amesema kuanzishwa kwa ushirika huo wa vijana wa ufugaji kuku mkoa wa Mjini Magharibi una lengo la kuhakikisha vijana wanajiongezea kipato na endelevu.

Pia amiomba serikali ya SMZ kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kuendeleza taifa .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmud, alisema mradi huo utawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kufikia uchumi wa kati.

"Mradii huu unatekelezwa kwa vitendo kwa kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira za serikali" alisema.

WAKULIMA WA MWANI WA KIJIJI CHA PAJE WAPATA KHOFU JUU YA KILIMO CHAO

Wakulima wa mwani wa kijiji cha paje wameuomba uongozi wa wizara ya kilimo kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuangalia harakati za watalii za michezo ya baharini katika fukwe za paje kwani zimeanza kuwajengea hofu juu ya kilimo chao cha mwani.

Wakulima hao wameiambia ZBC kuwa watalii wanafanya   michezo ya maputo smoklin karibu na maeneo ya fukwe wakati ambapo kilimo cha mwani kikiwa kinaendelea.

Wamesema kuwa ingawa utalii una faida sana katika taifa  lakini ni vyema taasisi husika zikakaa pamoja kuwapangia maeneo maalum ambayo wao watafanya michezo yao hiyo  na harakati za kilimo cha mwani zikiendelea.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema watakaa pamoja na mamlaka ya uwekezaji ili kutafuta muafaka wa tatizo hilo bila ya kutokea athari yoyote.

error: Content is protected !!