Category Archives: Biashara

habari za biashara

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIJANGWANI WAILILIA SERIKALI JUU YA HUDUMA ZA MAJI SAFI PAMOJA UMEME

Wafanyabiashara wa Soko la Kijangwani wameiomba Serikali kuwaekea Miundombinu mizuri katika Soko hilo ili waeweze kufanyabishara zao katika mazingira bora

Wakizungumza na Camera ya Habari za Biashara na Uchumi ya ZBC Wafanyabiashara hao wamesema eneo   waliohamishiwa kwa sasa ni Rafiki kwao kwa Biashara hivyo wameomba kuwekea Umeme na Huduma ya Maji safi na Salama

Aidha wameiomba Serikali kuwaweka katika  Eneo hilo kuwa Maalum katika kuendeleza Shughuli  zao za kufanya Biashara ili  kuepuka kuhamama kila sehemu jambo ambalo linawakimbizia Wateja wao katika Kazi zao.

Soko la Kijangwani limekuja kufuatia Serikali kuwaondosha Wafanyabiasha hao katika Soko la Darajani ili kuondoa msongamano ambao ungepelekea kuenea kwa Maradhi hatari ya Corona.

 

NMB BANK KUSAIDIA VIKUNDI VYA USHIRIKA KWA KUZINDUA PAMOJA AKAUNTI

Vikundi Elfu 28,000 vya Wanachama wa Kuweka na Kukopa ambavyo zipo Nje ya Mfumo Rasmi wa Huduma za Kifedha Nchini vinatarajiwa kufikiwa na Benki ya NMB  kwa kushirikiana na Kampuni ya Satf katika Kipindi cha Mwaka Mmoja ili kuhakikisha wanapata huduma za Kifedha.

 Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna wakati wa Uzindunzi wa NMB  Pamoja Akaunti ambapo Amesema Lengo la Akaunti hiyo ni Kuziba Pengo lililopo kati ya Taasisi za Fedha na Makundi yasiyo rasmi ya kuweka Akiba na Kukopa  kwa kuyasogezea Huduma za Kibenki karib

Nae Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za kati wa Benki ya NMB  Filbert Mponzi Amesema Akaunti hiyo ni Mahsusi kwa Wateja wa Benki hiyo na haina Makato ya Mwezi na Vikundi vinaweza kufungua Akaunti na kuweka Pesa kupitia Simu za Mkononi.

Kwa upande wao Baadhi ya vikundi vilivyoshiriki katika Uzinduzi huo wamesema Akaunti hiyo ni Mkombozi kwao kwani inaenda kuwapunguziia Gharama ya Usafiri kutafuta huduma za Kifedha.

NMB Pamoja Account ni mahsusi kwa Ajili ya Vyama vya Kuweka na Kukopa Vijijini ,  Vyama vya Kijamii vya Akiba, Benki za Kijamii Vijijini (Vicoba), Vikundi vya Kijamii vya Akiba, Mashirika ya Kijamii, Makundi ya Familia na Marafiki na Kuyaunganisha na Benki hiyo.

 

MADALALI WA SAMAKI SOKO LA KIHINANI KUCHUKULIWA HATUA

Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi imesema itawachukulia hatua za kisheria baadhi ya Madalali wa Samaki katika Soko la Kihinani ambao hawachukui tahadhari dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkuu wa Mkoa  huo  Mhe. Hassan Khatib  Hassan ameeeleza hayo wakati wa ziara katika eneo la Mnada huo akiwa pamoja na Viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Magharibi ‘a’, kuangalia utekelezaji wa hatua zinazochukuliwa na Wafanyabiashara hao kuhusu Kujikinga ya Maradhi hayo.

Amesema licha ya hatua zinazochukuliwa na Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa bado kuna baadhi ya Watu wanakwenda kinyume na maelekezo hayo.

Viongozi wa Mnada wa Soko la Samaki la Kihinani wamesema wataendelelea kushirikiana na Serikali kusimamia maelekezo na Maagizo yalitotolewa ikiwemo kutumia Vifaa Kinga na kutoa Elimu ya Kujikinga kwa Wafanyabiashara na wateja katika Eneo hilo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharibi ‘a’ Amour Ali Mussa amesema  hatua mbali mbali wamechukua ya kukutana na makundi  tofauti na  kuwapatia Elimu ya  kujikinga na Virusi vya Corona lakini muitikio bado  unaonekana ni mdogo.

 

SUKARI DAR BADO NI TATIZO

Upatikanaji wa Bidhaa ya Sukari katika Jiji la Dar es salaam bado ni tatizo kutokana na baadhi ya Wafanyabiashara kuuza kwa Shilingi Elfu tatu hadi Elfu nne badala ya Shilingi Elfu mbili mia sita kwa kilo.

Wakizungumza na ZBC  baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamesema hali hiyo imepelekea kushindwa kununua bidhaa hiyo muhimu hususani katika kipindi hicho cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara Wamesema baada ya kutangazwa kwa Bei elekezi  ya upatikanaji wa bidhaa hiyo umekuwa ni washida katika  Maduka  ya Jumla.

ZBC ilipita katika Maduka ya Jumla ya kuuza Sukari Jijini hapo nakushuhudia Matangazo katika Maduka hayo yakionyesha kutopatikana na Bidhaa hiyo.

Ikumbukwe hivi karibuni Serikali ilitangaza Bei elekezi ya Uuzaji wa Sukari Nchini ambapo kwa Mkoa Dar es salaam inatakiwa kuuzwa kwa Shilingi Elfu Mbili na Mia Sita na Shilingi Elfu tatu na mia mbili kwa baadhi ya Maeneo ya Nchi.