Serikali imewahimiza Wajasiriamali kujipanga na kuingia katika Mfumo Rasmi unaotambulika ili waweze kutambulika na kunufaika na fursa za kibiashara zinazoandaliwa na Serikali ili kukuza Biashara zao.
Tamko hilo limetolewa na kaimu Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mh Mudrik Soraga wakati akifunga Tamasha la saba la Biashara Maalum kwa Kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar katika Viwanja vya Maisara na kusema kufanya hivyo kutawasaidia kupata masoko , kupanua wigo wa Washirika wa Biashara pamoja na Serikali kujua Takwimu sahihi na mahoitaji ya Wajasiriamali waliop Nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda nd Juma Reli amesema Serikali inakusudia kuanzisha eneo Maalum la kudumu kwa ajili ya Tamasha la biashara kutokana na mafanikio yanayopatikana na ongezeko la idadi ya Wafanya biashara wanaojittokeza kila mwaka .
Ufungaji huo wa Tamasha la saba la Biashara uliambatana na utoaji wa vyeti Maalum kwa kampuni zilizojitokeza kudahmini Tamasha hilo na Taasisi zilizofanya vizuri katika Tamasha hilo lililo washirikisha Wafanya biasahara zaidi ya mia tatu .